
xxxxxxxxxxxxxxxxxx Mama Samia Legal Aid Campaign Yaweka Kambi Arusha. Timu ya watoa Huduma za Msaada wa Kisheria kupitia Kampeni ya "Mama Samia Legal Aid" imeweka kambi rasmi Machi 27, 2025 Jijini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa kuihudumia Jamii inayokabiliwa na uhitaji wa Msaada wa Kisheria. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewashauri watumishi wa Samia Legal Aid kuwa wasikivu na kutanguliza utu wanaposhughulikia kero za Wananchi, kwani wanamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye shauku yake kubwa ni Wananchi kutatuliwa changamoto zao. "Mnatakiwa kuwa wasikivu na kutanguliza utu mnaposhughulikia kero za wananchi, kwani mnamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye shauku yake kubwa ni wananchi kutatuliwa changamoto zao." Mhe. Makonda amesema hayo wakati akiongea na wataalam wa Sheria wakiwemo mawakili, maofisa maendeleo ya jamii pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali waliokutana kwaaajili ya kupanga mikakati ya utatuzi wa cha...