Posts

Showing posts from 2019

NAIBU KATIBU MKUU MPANJU: VIONGOZI WA DINI HAMASISHENI WANANCHI KUSAJILI WATOTO

NAIBU KATIBU MKUU MPANJU ATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI KUHAMASISHA WANANCHI KUSAJILI WATOTO ILI KUPATIWA VYETI VYA KUZALIWA

Image
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Amon Mpanju awaomba viongozi wa dini na kuwataka watendaji wa Serikali kuhamasisha waumini na wananchi waliopo maeneo yao kupeleka watoto kusajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Mpanju ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano katika mikoa ya Morogoro na Pwani uliofanyika wiki hii katika viwanja vya uwanja wa ndege Mkoani Morogoro. “Nitoe wito kwa viongozi wa dini zetu popote walipo kwenye mikoa ya Morogoro na Pwani, viongozi wa kijamii, wenyeviti wetu wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji waliochaguliwa hivi karibuni na watendaji kwa ngazi zote kuhakikisha mnahamasisha wananchi wetu kwenye mikoa hii wajitokeze katika kampeni inayoendelea kuwasajili watoto na kupatiwa cheti bure”alisema. Aidha ndg Mpanju aliwaeleza viongozi hao kwamba zoezi hilo linagusa mtoto aliyezaliwa mwishoni mwa mwaka 2014 mpaka wanaozaliwa sasahivi hivyo, w

MKUTANO WA WATAALAM WA SHERIA WA NCHI ZA SADC WAMALIZIKA

Image
Mwenyekiti wa mkutano wa wataalam wa sheria wa nchi za SADC ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na wajumbe baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizindua zoezi la uandikishaji wa watoto wa umri chini ya miaka mitano na ugawaji wa vyeti kwa watoto hao katika mikoa ya Morogoro na Pwani  uliofanyika katika viwanja vya uwanja wa Ndege Mkoa wa Morogoro.   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akionesha cheti cha kuzaliwa kwa wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa uandikishaji wa watoto wa umri chini ya miaka mitano na ugawaji wa vyeti kwa watoto hao katika mikoa ya Morogoro na Pwani. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Amon Mpanju akiongea na wananchi kwenye uzinduzi wa uandikishaji wa watoto wa umri chini ya miaka mitano na ugawaji wa vyeti kwa watoto hao katika mikoa ya Morogoro na Pwani.   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiangalia cheti cha kuzaliwa mtoto baada ya kuandikishwa  kwenye uzinduzi wa uandikishaji wa watoto wa umri chini ya miaka mitano na ugawaji wa vyeti kwa watoto hao kati

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUZINGATIA WELEDI WA TAALUMA ZAO

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi y a Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. ( Mst ), Mhe. George H. Mkuchika akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. ( Mst ), Mhe. George H. Mkuchika (katikati mstari wa mbele) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa  (wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele), Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Jaji Mathew Mwaimu (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma, baada ya ufunguzi wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma. Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali za Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawa

KATIBU MKUU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA AONGOZA MKUTANO WA WATAALAM WA SHERIA WA NCHI ZA SADC

Image
Mwenyekiti wa mkutano wa wataalam wa Sheria wa nchi za SADC ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kulia) akiongea na wataalam hao (hawapo pichani). Tanzania ni Mwenyekiti wa mkutano huo hivyo kumwezesha Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria kuwa Mwenyekiti wa mkutano huo. Mwenyekiti wa mkutano wa wataalam wa Sheria wa nchi za SADC ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA INAWATAKIA WATANZANIA WOTE HERI YA MIAKA 58 YA UHURU

Image

SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU KUADHIMISHWA KITAIFA DESEMBA 11 MWAKA HUU.

Image
Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwafahamisha kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yanayotarajiwa kufanyika Desemba 11, Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju na Kulia ni Kamishna wa Maadili na Viongozi wa Umma Mhe. Jaji mstaafu Harold Nsekela. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju akiongea waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwafahamisha kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yanayotarajiwa kufanyika Desemba 11 Jijini Dodoma. Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  Mhe. Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwafahamisha kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu. Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika wakati akiongea na waandishi wa hab

WAZIRI MAHIGA ASHUHUDIA UANDIKISHAJI VIZAZI, VIFO NA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO MKOANI IRINGA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mzazi cheti cha kuzaliwa mtoto baada ya kuandikishwa. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akionesha cheti cha kuzaliwa kilichoandikishwa. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi Emmy Hudson (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Bi. Lina Msanga katika zoezi la uandikishaji wa vizazi na vifo Mkoani Iringa.

DKT MAHIGA AWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA KIKAMILIFU ZOEZI LA USAJILI WA VIFO NCHINI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA na viongozi wa Mkoa wa Njombe baada ya kikao cha tathmini cha viongozi kuhusu mpango wa maboresho na usajili wa vifo katika Mkoa huo. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiongea na viongozi wa Mkoa wa Njombe kuhusu mpango wa Maboresho na usajili wa vifo katika Mkoa huo. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini Bi. Emmy Hudson akiongea kwenye kikao cha tathmini cha viongozi wa Mkoa wa Njombe kuhusu mpango wa maboresho na usajili wa vifo Mkoani humo. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Dkt Mahiga awataka watendaji wa Serikali kusimamia kikamilifu usajili wa vifo nchini Licha ya kuwepo kwa faida nyingi za usajili wa vifo nchini, lakini kumekuwepo na mwamko mdogo wa wananchi kuona umuhimu wa zoezi hilo mara baada ya kifo. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi yao, idadi ya vifo nchini  vilivyosajiliwa inaonesh

Dkt Mahiga Awataka Wakuu wa Magereza Nchini Kutumia Ujuzi wa Wafungwa Kujiendesha na Kutoa Mchango wa Gawio kwa Serikali

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea gereza la Mahabusu Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wakati akiendelea na ziara yake. Viongozi mbalimbali walioambatana na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakiingia kwenye gereza la  Mahabusu Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya . XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Balozi Dkt Augustine Mahiga amewataka Wakuu wa Magereza nchini kutumia nguvu kazi na ujuzi wa wafungwa walioko magerezani kubuni miradi mbalimbali ili kuwazalishia fedha zitakazowawezesha kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini. Balozi Mahiga ameyasema hayo leo alipotembelea gereza la Kyela kujionea jinsi Taasisi za Haki Jinai zinavyotekeleza majukumu yake katika mahakama na magereza ikiwemo kutatua changamoto ya mrundikano wa mahabusu katika magereza pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji haki na hali ya magereza kote nchini. “Nguvu ka

SERIKALI YATAIFISHA MAGARI MANNE NA PIKIPIKI 16 KWA KOSA LA KUJIHUSISHA NA UHALIFU JIJINI MBEYA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiangalia magari yaliyotaifishwa na Serikali kwa kosa la kujihusisha na uhalifu mbalimbali wakati akiendelea na ziara yake jijini Mbeya.

DPP afuta Kesi 59 zaidi jijini Mbeya

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Chalya J. Nyangidu (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka Biswalo Mganga (wa pili kulia), walipotembelea Ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya leo tarehe 28 Nov. 2019 wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) akisalimiana na afisa wa magereza wakati wa ziara ya kikazi katika gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe Jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Tukuyu ASP. Samwel J. Kaluwa akiwatambulisha Staff wa gereza hilo mbele ya Waziri. Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) kulia akiwa na mwenyeji wake Kamishna Msaidizi wa Magereza Mkoa wa Mbeya Mathias   Mkama (ACP) katikati, alipotembelea Gereza Kuu la Ruanda Mbeya 27 Nov. 2019. Kushoto ni Kamishna Msaidizi   wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ruanda Mbeya Vendeline Tesha wakati wa ziara ya kikazi jiji

RAIA WA ETHIOPIA WALIOMALIZA VIFUNGO WARUDI NCHINI KWAO – WAZIRI MAHIGA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ataka raia wa Ethiopia waliomaliza vifungo vyao warudishwe nchini kwao. Waziri Mahiga ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ya siku saba katika Mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya ambapo anatembelea magereza ili kuona Haki Jinai inavyotekelezwa katika mikoa hiyo. “Hakuna sababu kwa nini raia hawa waendelee kutumia gharama kubwa ya Serikali yetu wakati wameshamaliza vifungo vyao, naahidi kuwa tutatumia kila njia kuhakikisha Serikali inatua mzigo huu”, alisema Balozi Mahiga. Akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Ndg. Biswalo Mganga, Waziri Mahiga alianza ziara yake kwa kutembelea gereza la Wilaya ya Iringa mjini na kujionea namna Haki Jinai inavyotekelezwa katika gereza hilo. Waziri Mahiga alizipongeza taasisi za Haki Jinai Mkoani humo kwa kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha haki jinai inatekelezwa ipasavyo na kuepuka vitendo vya rushwa, unyanyasaji na ubambikizaji wa kesi kwa watuhumiwa.

MAFANIKIO YA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA SEKTA YA SHERIA

Image
Kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama Kuu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Sheria ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

MWENYEKITI TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA AMTEMBELEA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA OFISINI KWAKE

Image
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga baadhi ya machapisho kutoka tume katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria. Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Mahiga akiongea na ujumbe waTume ya Haki za Binadamu na Utawala bora uliotembelea ofini kwake mapema Novemba 18, 2019. Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kulia kwake). Wengine ni Makamishna wa Tume, kutoka kulia ni Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa, Thomas Masanja, Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan na Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli

HABARI PICHA: WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKIPANDA MITI KATIKA ENEO LA WIZARA

Image
DODOMA: Katika juhudi za kumuunga Mkono Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Dodoma kuwa ya kijani Waziri wa katiba na Sheria Dr. Balozi Agostino Mahiga kwa kushirikiana na Watumishi wa Wizara wamefanya zoezi la upandaji miti katika eneo la Wizara hiyo. Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria {wa kwanza} Prof. Sifuni Mchome akimuongoza Waziri wa Katiba na Sheria kuelekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya upandaji miti Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo. Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {kushoto} akichagua miti kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti katika maeneo ya Wizara  Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo. Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {katikati} akiandaa shimo kabla ya kupanda mti katika eneo la ofisi za Wizara  Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {katikati} akipanda mti katika eneo la ofisi za

Wizara ya Katiba Yaunga Mkono Kampeni ya Kuikijanisha Dodoma

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani.