Friday, November 29, 2019

DPP afuta Kesi 59 zaidi jijini MbeyaWaziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Chalya J. Nyangidu (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka Biswalo Mganga (wa pili kulia), walipotembelea Ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya leo tarehe 28 Nov. 2019 wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo.


Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) akisalimiana na afisa wa magereza wakati wa ziara ya kikazi katika gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe Jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Tukuyu ASP. Samwel J. Kaluwa akiwatambulisha Staff wa gereza hilo mbele ya Waziri.Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) kulia akiwa na mwenyeji wake Kamishna Msaidizi wa Magereza Mkoa wa Mbeya Mathias  Mkama (ACP) katikati, alipotembelea Gereza Kuu la Ruanda Mbeya 27 Nov. 2019. Kushoto ni Kamishna Msaidizi  wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ruanda Mbeya Vendeline Tesha wakati wa ziara ya kikazi jijini humo.     XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Katika mwendelezo wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) kwenye Mikoa ya kusini, Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka Tanzania (DPP) Biswalo Mganga amefuta jumla ya kesi 59 katika mahakama za Mkoa wa Mbeya.

Mkurugenzi Biswalo ameyafanya hayo katika gereza la Ruanda mjini Mbeya na gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe alipoambatana na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Mahiga ili kujionea hali halisi ya mazingira ya utoaji haki jinai katika magereza hayo na taasisi mbalimbali za haki jinai ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Polisi, Mahakama na Magereza yenyewe.

“Niliowafutia Kesi nendeni mkawe raia wema, msirudie makosa, badala yake mkawe mabalozi wema mtakaofanya kazi kwa bidii ili kumuunga mkono Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kauli yake ya hapa kazi tu.”

Kwa upande wake Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) aliwataka wote waliofutiwa mashitaka kwenda kufurahi na familia zao huku wakimshukuru Mungu na kujutia makosa yaliyosababisha kushitakiwa kwao. Aidha, aliwaonya kutokurudia makosa hayo badala yake watumie nguvu na akili walizonazo kuzalisha mali kwa maendeleo yao na familia zao pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.

“Mliosamehewa leo nendeni mkafurahi na familia zenu sambamba na kuwa watu wema katika jamii inayowazunguka kwani ni matumaini yangu kuwa mmejifunza mengi na mmebadilika. Kuna watu hapa nikiwatizama misuli yao, walipaswa wakaitumie kufanya kazi na kuzalisha mali kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla badala ya kuitumia kufanya uhalifu.”

Kwa mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo 2002, Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka anayo mamlaka ya kuwafutia mashitaka watuhumiwa wa makosa ya jinai katika magereza mbalimbali nchini. Mpaka sasa katika ziara hii ya kikazi ya Waziri wa Katiba na Sheria katika Mikoa mitatu DPP Biswalo ameshafuta  jumla ya kesi 120 na bado ziara inaendelea katika Wilaya ya Kyela na baadae Mkoa wa Njombe.Tuesday, November 26, 2019

RAIA WA ETHIOPIA WALIOMALIZA VIFUNGO WARUDI NCHINI KWAO – WAZIRI MAHIGAWaziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ataka raia wa Ethiopia waliomaliza vifungo vyao warudishwe nchini kwao.

Waziri Mahiga ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ya siku saba katika Mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya ambapo anatembelea magereza ili kuona Haki Jinai inavyotekelezwa katika mikoa hiyo.

“Hakuna sababu kwa nini raia hawa waendelee kutumia gharama kubwa ya Serikali yetu wakati wameshamaliza vifungo vyao, naahidi kuwa tutatumia kila njia kuhakikisha Serikali inatua mzigo huu”, alisema Balozi Mahiga.

Akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Ndg. Biswalo Mganga, Waziri Mahiga alianza ziara yake kwa kutembelea gereza la Wilaya ya Iringa mjini na kujionea namna Haki Jinai inavyotekelezwa katika gereza hilo.

Waziri Mahiga alizipongeza taasisi za Haki Jinai Mkoani humo kwa kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha haki jinai inatekelezwa ipasavyo na kuepuka vitendo vya rushwa, unyanyasaji na ubambikizaji wa kesi kwa watuhumiwa.

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Ndg. Biswalo Mganga katika ziara hiyo ametumia mamlaka yake kisheria kufuta kesi 45 ambazo ziko mahakama za mwanzo na Wilaya na ameahidi kuendelea kufanya hivyo kwa kesi nyingine. Mkurugenzi Mganga alifikia uamuzi wa kufuta kesi hizo baada ya kupitia mafaili na kujiridhisha kuwa hakuna haja ya kuendelea na kesi hizo lengo ikiwa ni kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati.


Monday, November 25, 2019

MAFANIKIO YA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA SEKTA YA SHERIA

Kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama Kuu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Sheria ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Friday, November 22, 2019

MWENYEKITI TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA AMTEMBELEA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA OFISINI KWAKE


Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga baadhi ya machapisho kutoka tume katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria.Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Mahiga akiongea na ujumbe waTume ya Haki za Binadamu na Utawala bora uliotembelea ofini kwake mapema Novemba 18, 2019.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kulia kwake). Wengine ni Makamishna wa Tume, kutoka kulia ni Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa, Thomas Masanja, Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan na Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli

Wednesday, November 20, 2019

HABARI PICHA: WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKIPANDA MITI KATIKA ENEO LA WIZARA

DODOMA: Katika juhudi za kumuunga Mkono Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Dodoma kuwa ya kijani Waziri wa katiba na Sheria Dr. Balozi Agostino Mahiga kwa kushirikiana na Watumishi wa Wizara wamefanya zoezi la upandaji miti katika eneo la Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria {wa kwanza} Prof. Sifuni Mchome akimuongoza Waziri wa Katiba na Sheria kuelekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya upandaji miti Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {kushoto} akichagua miti kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti katika maeneo ya Wizara  Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {katikati} akiandaa shimo kabla ya kupanda mti katika eneo la ofisi za Wizara  Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {katikati} akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara  Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {kushoto} akimwagilia mti baada ya kuupanda katika eneo la ofisi za Wizara  Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari (HGCU) wa Wizara ya Katiba na Sheria Karimu Meshack akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara  Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi (Dereva) wa Wizara ya Katiba na Sheria Kassim Abdallah akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.

Wizara ya Katiba Yaunga Mkono Kampeni ya Kuikijanisha DodomaKatibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo. Zoezi hilo ni jitihada za Wizara hiyo katika kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais ya kuifanya Dodoma inakuwa ya kijani.