HABARI PICHA: WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKIPANDA MITI KATIKA ENEO LA WIZARA
DODOMA: Katika juhudi za kumuunga Mkono Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Dodoma kuwa ya kijani Waziri wa katiba na Sheria Dr. Balozi Agostino Mahiga kwa kushirikiana na Watumishi wa Wizara wamefanya zoezi la upandaji miti katika eneo la Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria {wa kwanza} Prof. Sifuni Mchome akimuongoza Waziri wa Katiba na Sheria kuelekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya upandaji miti Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {kushoto} akichagua miti kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti katika maeneo ya Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {katikati} akiandaa shimo kabla ya kupanda mti katika eneo la ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {katikati} akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt Balozi Agostino Mahiga (Mb) {kushoto} akimwagilia mti baada ya kuupanda katika eneo la ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari (HGCU) wa Wizara ya Katiba na Sheria Karimu Meshack akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi (Dereva) wa Wizara ya Katiba na Sheria Kassim Abdallah akipanda mti katika eneo la ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo.
Comments
Post a Comment