WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUZINGATIA WELEDI WA TAALUMA ZAO
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (katikati mstari wa mbele) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele), Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Jaji Mathew Mwaimu (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma, baada ya ufunguzi wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali za Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika wakati akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Watumishi wa Umma wametakiwa kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao.
kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kepteni Mstaafu George Mkuchika
wakati akifungua maadhimisho ya siku ya maadili
na haki za bianadamu kitaifa jijini Dodoma ambapo amewataka watumishi wa Umma
kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili.
“Tunaona Maadili ndio neno la Msingi Miongoni mwa jitihada za serikali ni kutunga
sheria na kanuni mbalimbali zinazozingatia Maadili na Kanuni za utumishi wa
umma, hivyo
niwaase watumishi wa umma kuzingatia katika kufuata na kusimamia sheria
na Miongozo ya utumishi kwa lengo la kuboresha utawala bora” amesema.
Aidha, Waziri
Mkuchika amesema suala la mfumo wa Mtandao limekuwa na mchango mkubwa katika
kuhakiki watumishi feki pamoja na uadilifu wa matumizi ya fedha za umma.
Awali akizungumza katika
maadhimisho hayo, Naibu
Waziri Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mary Mwanjelwa amesema kuwa Serikali
ya Awamu ya Tano imejikita katika masuala ya uadilifu na uzalendo hivyo kila mmoja
anapaswa kuepuke kufanya
mambo yasiyofaa katika taifa.
“Sisi tunatakiwa kuwa mfano bora
katika kusimamia uadilifu na utawala bora hivyo niwaase watumishi wa umma kuwa
jambo la uadilifu ni jambo la muhimu sana”
Kwa upande wake Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili
ya viongozi wa Umma Jaji Mstaafu
Harold
Nsekela ameelezea chimbuko la siku hiyo kuwa ni siku ya kimataifa ya kuzuia na
kupambana na Rushwa ambayo huadhimishwa
Desemba 09 ya kila mwaka
Tangu mwaka 2017 maadhimisho ya siku
ya maadili na haki za bianadamu kitaifa yamekuwa yakifanyika Jijini Dodoma
kufuatia maamuzi ya Serikali kuhamishia makao makuu jijini hapa na kauli mbiu
kwa mwaka huu ni “Maadili
katika Utumishi
wa Umma ni Nguzo
Muhimu katika Kuimarisha
Utawala Bora na Haki za Binadamu”
Comments
Post a Comment