WANYONGE NI LAZIMA WALINDWE NA SHERIA-DKT MWIGULU

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiongea na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiongea na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli imejipambanua kuwalinda wanyonge hivyo anapojitokeza mtu yeyote kutaka kuwaumiza ni lazima ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ametoa angalizo hilo tarehe 15 Disemba 2020 wakati akizungumza kwenye kikao kazi na kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Anamringi Macha akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga. Nchemba amekemea vikali wananchi wanaotaka kuijaribu serikali inay...