WIZARA YA KATIBA NA SHERIA WAFANYA UCHAGUZI KUPATA WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Deogratias Yinza akiongoza kikao cha uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Antelmas Tarimo (aliyesimama) akitoa sifa za wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kabla ya uchaguzi wa wajumbe wa baraza hilo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakisikiliza maelekezo kabla ya kufanya uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi.
Msimamizi wa uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Neema Dickson (kulia) akisimamia zoezi la kuhesabu kura.
Msimamizi wa uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Neema Dickson akitangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Antelmas Tarimo (aliyesimama) akitoa sifa za wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kabla ya uchaguzi wa wajumbe wa baraza hilo.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakisikiliza maelekezo kabla ya kufanya uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi.
Msimamizi wa uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Neema Dickson akitangaza matokeo ya uchaguzi huo.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Deogratias Yinza awataka
wajumbe waliochaguliwa kuwawakilisha wenzao kwenye baraza la wafanyakazi
kuhakikisha wanawakilisha vyema mawazo ya wenzao waliowachagua.
Hayo ameyasema kwenye zoezi la
uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo baada ya wajumbe wa
awali kumaliza muda wao mwishoni mwa mwaka jana.
“Wawakilishi mliochaguliwa
kuwawakilisha wenzenu kwenye baraza la wafanyakazi mhakikishe mnawakilisha
vyema mawazo ya waliowachagua” alisema.
Aidha, Katibu wa TUGHE Mkoa wa
Dodoma Bw. Antelmas Tarimo alitaja sifa za mjumbe wa baraza ikiwmo mtu
anayejitambua, anayejitoa na mchapakazi, pia awe anajua baadhi ya mambo ya
kisheria na utumishi ili kumwezesha kuhoji vizuri mambo muhimu mfano haki za
watumishi.
Aliongeza, wajumbe wazuri
wanaotoa mawazo ya kusaidia taasisi ni muhimu kwenye baraza na sio kuangalia
urafiki ili kuboresha maslahi na utendaji wa taasisi.
“Usichague mtu sababu ni rafiki
au mmezoeana”, alisema Tarimo.
Naye Afisa kazi Mkoa wa Dodoma
Bi. Neema Dickson ambaye ni msimamizi mkuu wa uchaguzio huo alisema
waliochaguliwa washiriki ipasavyo kuwawakilisha wenzao ili kutatua changamoto
zinazo wakabili na kuwakilisha mawazo yao vyema kwa viongozi wa baraza.
Katika uchaguzi huo kila Idara na
Kitengo ilichagua mjumbe ambaye ana jukumu la kuwasilisha mawazo na maoni yake
pamoja na ya wenzake katika kikao cha baraza la wafanyakazi kinachofanyika kila
mwaka.
Comments
Post a Comment