OFISI ZA KATA KUTUMIKA KUSAJILI WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akitoa elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Korona kwa wananchi waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma kusajili wa watoto walio chini ya Miaka Mitano unaofanywa na RITA. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akishuhudia zoezi la usajili wa watoto chini ya umri wa miaka mitano katika kituo cha usajili kilichopo katika Hospitali ya Misheni Peramiho Mkoa wa Ruvuma. Baadhi ya Wazazi wakionesha vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao walivyokabidhiwa na Naibu Katibu MKuu wa Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju baada ya kufanikiwa kuwasajili watoto wao. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini RITA umefanya maboresho ya mfumo wa usajili kuwezesha Vituo vya Afya pamoja ofisi za kata vitumike kuwasajili watoto na kupatiwa cheti cha kuzaliwa. Hayo yameelezwa jana na Msajili wa Vizazi na Vifo na Mratibu wa zoezi la U...