MWIGULU ATAKA HAKI ZA BINADAMU ZILINDWE

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akipokea maua kutoka kwa Wakili wa Serikali Bi. Esther Msambazi alipofika kwa mara ya kwanza Wizarani hapo baada ya kuapishwa jana kuiongoza wizara hiyo.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akiwa Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma kwa mara ya kwanza, baada ya kuapishwa jana kuiongoza wizara hiyo.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akiwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi katika kikao kifupi cha ukaribisho aliporipoti ofisini kwake leo (Mei 04/2020) Mtumba, jijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akiwaongoza watumishi wa Wizara hiyo kumuombea mtangulizi wake aliyefariki hivi karibuni.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX



Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amesema atasimamia yale ambayo ana hakika ni matamanio ya  Rais Magufuli kuona yakitekelezwa kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ikiwemo kuona haki za binadamu hazipotei.

Akizungumza leo Mei 4, 2020 aliporipoti  ofisini kwake baada ya kuteuliwa na Rais kushika wadhifa huo na kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo katika kikao kifupi cha ukaribisho Waziri Nchemba amesema  “Tupo kwenye Wizara ambayo ipo kwenye maeneo ambapo nna hakika Rais ameandika moyoni mwake kuona yakilindwa ikiwemo kuona haki za binadamu hazipotei”

Amesema, ni lazima katika majukumu ya Idara na Vitengo vyetu tulipe  kipaumbele suala hili na kuhakikisha linafanikiwa.

Mbali na kutaka upatikanaji wa haki za binadamu uzingatiwe Waziri Nchemba alisisitiza watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili kuleta matokeo yanayotarajiwa na Rais na pia kulinda rasilimali zilizopo.

Waziri Nchemba aliwaomba watumishi kuendeleza ushirikiano uliokuwepo tangu enzi za mtangulizi wake na kuchapa kazi kwa juhudi zote. Pia aliwataka kuangalia maeneo mapya na kuibua fursa mbalimbali zitakazoleta tija katika Wizara hiyo.

Aidha, awali akimkaribisha Waziri Nchemba, Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome alimueleza Waziri huyo kuwa  watumishi wapo tayari kushirikiana nae na kuunga mkono juhudi za Rais za kuliletea maendeleo Taifa letu.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA