WIZARA YA KATIBA YAENDELEA KUIKIJANISHA DODOMA

Mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Dina Njovu akisukuma toroli kupeleka miti kwenye mashimo ili iweze kupandwa. Mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Ernest Mbuna akimwagilia maji mti aliopanda katika zoezi la upandaji miti lililofanyika leo katika viwanja vya Wizara hiyo. Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Deogratias Yinza akichimba shimo kwa ajili ya kupanda ua katika eneo linalozunguka ofisi za Wizara hiyo. Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika zoezi la upandaji miti na maua katika eneo llinalozunguka ofisi hizo leo Mtumba jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Wizara ya Katiba na Sheria yaendelea kuikijanisha Dodoma kwa kupanda miti ya kivuli, matunda na maua katika viwanja vya Wizara hiyo iliyopo Mtumba Mkoani Dodoma. Zoezi hilo la upandaji miti limekuwa likifanyika mara kwa mara ili kuwezesha viwanja vya wizara hiyo kuwa na mazingira mazuri ya kuvutia. Miti hiyo mbali na kuw...