WIZARA YA KATIBA YAENDELEA KUIKIJANISHA DODOMA
Wizara ya Katiba na Sheria yaendelea kuikijanisha Dodoma kwa
kupanda miti ya kivuli, matunda na maua katika viwanja vya Wizara hiyo iliyopo Mtumba Mkoani Dodoma.
Zoezi hilo la upandaji miti limekuwa likifanyika mara kwa
mara ili kuwezesha viwanja vya wizara hiyo kuwa na mazingira mazuri ya kuvutia.
Miti hiyo mbali na kuwapatia kivuli, watumishi watapata
fursa ya kula matunda mbalimbali wakiwa kazini ikiwemo zabibu ambalo ni zao
linalostawi sana mkoani Dodoma.
Aidha Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara
hiyo Ndg. Deogratias Yinza amekuwa mstari wa mbele katka kuhamasisha upandaji
wa miti katika maeneo ya viwanja vya
Wizara hiyo na hivyo kuwapa mwamko watumishi wa wizara hiyo wa kupanda miti ili
kukabiliana na hali ya ukame iliyopo katika Mkoa wa Dodoma.
Zoezi hili la upandaji miti limejumuisha watumishi wote wa
Wizara ya Katiba na Sheria.
Comments
Post a Comment