Posts

Showing posts from August, 2020

WATAALAM WA SHERIA KUTOKA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA NA TAASISI NYINGINE WAJADILIANA KUHUSU MAREKEBISHO YA SURA YA 16

Image
Wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara na Taasisi nyingine za Serikali wakiwa katika majadiliano ya mapitio ya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16. wataalam hao walianza kupitia vifungu kimoja baada ya kingine vya sura ya 16 katika mafungu waliyogawana na sasa wanaendelea na majadiliano ya namna ya kuvirekebisha vifungu vilivyoonekana vinamapungufu na haviendani na wakati wa sasa. 

WADAU WA UJENZI WA AMANI WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Wananchi wa Ngorongoro wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa kujenga na kudumisha amani nchini.   Wameyasema hayo wakati wa Kikao na Kamati ya Kitaifa ya Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya Kimbari kilichofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Mji mdogo wa Loliondo jijini Arusha.   Katika kikao hicho kilichohusisha viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Wadau wa Amani ambao ni wakulima na wafugaji katika Wilaya hiyo pamoja na Wataalamu wa Kamati ya Kitaifa ya Amani kimelenga kubaini viashiria au vyanzo vya migogoro inayohusisha rasilimali na kusababisha uvunjifu wa amani ili kuitafutia suluhisho la kudumu kabla haijaleta madhara kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.   “Tunamshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake makini uliojaa busara na hekima na kuwezeha kuwa na amani katika jamii yetu. Siku hizi hatugombani na unaweza kuuza ng’o

KAMATI YA KUZUIA MAUAJI YA KIMBARI YAMTEMBELEA MKUU WA MKOA ARUSHA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta akiongea na kamati ya kuzuia mauaji ya Kimbari ilipomtembelea ofisini kwake jijini Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta akiongea na wajumbe wa kamati ya kuzuia mauaji ya Kimbari ilipomtembelea ofisini kwake. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Kamati ya Kitaifa ya Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya Kimbari inayongozwa na Felistas Mushi (Mwenyekiti) kutoka Wizara ya Katiba na Sheria imetembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha.   Kamati hiyo  ya watalaamu watano imefika kwa Mkuu wa Mkoa Mh. Idd Hassan Kimanta kujitambulisha kabla ya kuanza utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya Ujenzi wa Amani Nchini katika Mkoa wa Arusha katika maeneo amabayo yamekuwa yakikumbwa na migogoro inayohusisha rasilimali na hatimaye kusababisha mapigano na mauaji kati ya wakulima na wafugaji, wawekezaji na wananchi na wakati mwingine wananchi wenyewe kwa wenyewe.    Kamati hii iliundwa mwezi  Februari, 2012 chini ya Itifa

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAFANYA MAPITIO YA SHERIA YA KANUNI YA ADHABU SURA YA 16

Image
 Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Bw. Patience Ntwina akitoa maelezo kwa watalaam wa kikao kazi kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali wanaofanya mapitio ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mjini Morogoro.  Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Bw. Patience Ntwina akitoa maelezo kwa watalaam wa kikao kazi kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali wanaofanya mapitio ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mjini Morogoro. Wataalam wakiendelea na majadiliano. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina afungua kikao kazi kuhusu mapitio ya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16. Kikao kazi hicho cha siku 12 kinafanyika katika ukumbi wa TFS-Mbegu mjini Morogoro kinajumuisha wataalam kutoka  Wizara, Idara na Taasisi za Serikali. Mkurugenzi Ntwina akizungumza na wataalam hao amesema “Wizara imepanga kufanya zoezi la mapitio ya sheria hii ili kuondoa maneno, maudh

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAJIPANGA KWA MABORESHO YA SEKTA YA SHERIA AWAMU YA PILI

Image
Mratibu wa programu ya maboresho ya sekta ya sheria Bw. Emmanuel Mayeji (kulia) akifuatilia majadiliano ya taarifa ya utafiti wa kuhakiki visababishi vya changamoto zinazoikabili sekta ya sheria nchini kwa ajili ya maandalizi ya andiko la awamu ya pili ya programu ya maboresho ya sekta ya sheria yaliyofanyika jijini Morogoro. Mwingine pichani ni Kaimu Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania ambaye ndiye alikuwa muongoza majadiliano hayo Dkt. Zakayo Lukumay. Mratibu wa programu ya maboresho ya sekta ya sheria Bw. Emmanuel Mayeji akichangia mada. Wakili wa Serikali Mwandamizi Bi. Anne Malipula akichangia mada. Wadau mbalimbali wakifuatilia majadiliano. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Wizara ya Katiba na Sheria yajipanga kwa maboresho ya sekta ya sheria awamu ya pili kwa kujadili taarifa ya utafiti wa kuhakiki visababishi vya changamoto zinazoikabili sekta ya sheria nchini. Majadiliano hayo ya siku moja  yamefanyika jijini Morogoro miongoni mwa wadau wa

DKT. MWIGULU NCHEMBA ATEMBELEA OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba akifafanua jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, jijini Dar es Salaam. Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Gabriel Malata (kulia) akimkabidhi taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Amon Mpanju (kushoto), jijini Dar es Salaam. Sehemu ya Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka watendaji wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuhakikisha haki inapatikana kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Akizungumza na menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo Dkt. Nchemba amesema, hatapenda kuona uzembe unafanywa na mawakili wasomi wa serikali katika kusimamia haki. “Mtendaji yoyote akifanya kosa ambalo litaleta madhara kwa taifa kupitia utendaji wake,

KIKAO CHA SADC SEKTA YA SHERIA CHAKUBALIANA UTAFITI UFANYWE KUGUNDUA KINACHOCHELEWESHA URIDHIWAJI WA ITIFAKI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akifungua kikao cha SADC  cha Mawaziri na Wanasheria Wakuu Ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar Es Salaam. Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akifungua kikao cha SADC  cha Makatibu Wakuu na Naibu Wanasheria Wakuu Ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar Es Salaam. Kikao cha SADC kwa sekta ya Sheria kikiendelea. Picha ya pamoja ya viongozi na wataalam baada ya kukamilika kwa kikao cha SADC cha sekta ya sheria, ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Darv Es Salaam. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye ni Mwenyekiti wa SADC kwa sekta ya sheria asema kikao cha SADC kwa sekta ya sheria kimekubaliana utafiti ufanywe ili kugundua kinachochelewesha uridhiwaji wa itifaki. Waziri Nchemba ameyasema hayo baada ya kumalizika kwa kikao cha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa nchi za SADC kilichofanyika jijini Dar Es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nye

MAANDALIZI YA MKUTANO WA SADC KWA SEKTA YA SHERIA

Image
Maandalizi ya mkutano wa SADC kwa sekta ya sheria unaotarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar Es Salaam yakiendelea