KIKAO CHA SADC SEKTA YA SHERIA CHAKUBALIANA UTAFITI UFANYWE KUGUNDUA KINACHOCHELEWESHA URIDHIWAJI WA ITIFAKI


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akifungua kikao cha SADC  cha Mawaziri na Wanasheria Wakuu Ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akifungua kikao cha SADC  cha Makatibu Wakuu na Naibu Wanasheria Wakuu Ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar Es Salaam.


Kikao cha SADC kwa sekta ya Sheria kikiendelea.

Picha ya pamoja ya viongozi na wataalam baada ya kukamilika kwa kikao cha SADC cha sekta ya sheria, ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Darv Es Salaam.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye ni Mwenyekiti wa SADC kwa sekta ya sheria asema kikao cha SADC kwa sekta ya sheria kimekubaliana utafiti ufanywe ili kugundua kinachochelewesha uridhiwaji wa itifaki.

Waziri Nchemba ameyasema hayo baada ya kumalizika kwa kikao cha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa nchi za SADC kilichofanyika jijini Dar Es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere.

Waziri Nchemba alisema katika kikao hicho wamekubaliana kutoweka ukomo wa uridhiwaji wa itifaki bali wafanye utafiti ili kujua sababu za ucheleweshwaji huo na japokuwa nchi zinatofautiana taratibu nyingine zinaenda Bunge na nyingine na Baraza la Mawaziri kwanza kujadiliwa kabla ya kuwasilishwa kikaoni, hivyo hiyo ni moja ya sababu ya ucheleweshwaji.

“ Tumekubaliana kutoweka ukomo wa uridhiwaji wa itifaki bali tujue tatizo la ucheleweshwaji” alisema Waziri Nchemba.

Katika majadiliano yao Waziri Nchemba amesema wamekubaliana masuala mengine kama takwimu yasubirie misimamo ya ndani ya nchi halafu ndipo iwasilishwe katika kikao ngazi ya Mawaziri na Wanasheria Wakuu ili yaweze kutolewa maaamuzi.

Aidha, Kabla ya kikao hicho kilitangulia kikao cha wataalam ngazi ya Makatibu Wakuu na Naibu Wanasheria Wakuu, walijadili mambo mbalimbali ikiwemo kasi ndogo katika uridhiwaji wa itifaki na waliona si jambo rahisi nchi zote kuamua kwa wakati mmoja hivyo kutokana na taratibu za ndani ya nchi kutofautiana, masuala ya kazi ambapoitifaki hii ilionekana ni ngumu kutekelezeka hivyo kikao kiliamua kuachana nayo na kutengeneza itifaki mpya.

Pia, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema katika kikao hicho kwa upande wa takwimu waliona kuna mambo hayajakamilika hivyo irudi katika ngazi ya wataalam ili yaweze kufanyiwa kazi kabla hayajaenda mbele kwa ajili ya maamuzi.

“ Kuna mambo ambayo bado hayajakamilika hivyo yarudi ngazi ya wataalam kabla hayajaenda mbele kwa ajili ya maamuzi”. Alisema Prof, Mchome.

Vilevile, itifaki nyingine iliyojadiliwa ni udhibiti wa silaha ndogo ambapo walikubaliana itifaki hii iwekewe muongozo ili kudhibiti uingizwaji wa silaha haramu na vyombo vya ulinzi vya nchi wanachama wa SADC vishirikiane kulinda amani na usalama wan chi.                                                                                                           

Akifunga kikao hicho Waziri Nchemba alisema ni kikao kizuri chenye tija, hakikuwa na mvutano wowote na mambo waliyokubaliana yaendelee na ambayo hayakukamilika yatarudi yafanyiwe kazi.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA