WADAU WA UJENZI WA AMANI WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Wananchi wa
Ngorongoro wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe
Joseph Magufuli kwa kujenga na kudumisha amani nchini.
Wameyasema hayo
wakati wa Kikao na Kamati ya Kitaifa ya Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya
Kimbari kilichofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro, Mji mdogo wa Loliondo jijini Arusha.
Katika kikao
hicho kilichohusisha viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Wadau wa
Amani ambao ni wakulima na wafugaji katika Wilaya hiyo pamoja na Wataalamu wa
Kamati ya Kitaifa ya Amani kimelenga kubaini viashiria au vyanzo vya migogoro
inayohusisha rasilimali na kusababisha uvunjifu wa amani ili kuitafutia
suluhisho la kudumu kabla haijaleta madhara kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Tunamshukuru
Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake makini uliojaa busara na hekima na kuwezeha
kuwa na amani katika jamii yetu. Siku hizi hatugombani na unaweza kuuza ng’ombe
hata 1000 na ukatembea huku umeshika pesa mkononi na ukawa salama jambo ambalo
halikuwepo hapo zamani Mbung’ai Ole Sasi.
Kwa upande wake
Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya Kimbari Bw.
Miraji Maira amewashukuru wadau wa Amani walioshiriki kwa kubainisha viashiria
vya migogoro na kuahidi kuyafanyia kazi. Aidha, Katibu Maira amesema
amefurahishwa kuona watu wanashuhudia kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais John
Pombe Joseph Magufuli na kuwataka waendelee kumuunga mkono kwa kuendelea
kujenga amani katika jamii kwani ni wajibu wao na ikitokea migogoro waitatue
kwa njia ya amani.
“Nimefurahi
kusikia hamgombani badala yake mnatatua changamoto zenu kwa amani, endeleeni
hivyo kwasababu wajibu wa kulinda amani upo mabegani mwenu, hakuna mtu mwingine
wa kuwatatulia migogoro yenu” amesema Miraji Maira.
Kamati ya Kitaifa
ya Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya Kimbari iliyoanzishwa Februari, 2012
chini ya itifaki ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na kuridhiwa na serikali ya
Tanzania kupitia Mkataba wa nchi za Maziwa Makuu wa Usalama, Utulivu na
Maendeleo kesho itaendelea na mkakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya msingi
ya kujenga na kudumisha amani na utengamano katika mikoa ya Manyara na baadae
Rukwa na Morogoro.
Comments
Post a Comment