WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAJIPANGA KWA MABORESHO YA SEKTA YA SHERIA AWAMU YA PILI

Mratibu wa programu ya maboresho ya sekta ya sheria Bw. Emmanuel Mayeji (kulia) akifuatilia majadiliano ya taarifa ya utafiti wa kuhakiki visababishi vya changamoto zinazoikabili sekta ya sheria nchini kwa ajili ya maandalizi ya andiko la awamu ya pili ya programu ya maboresho ya sekta ya sheria yaliyofanyika jijini Morogoro. Mwingine pichani ni Kaimu Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania ambaye ndiye alikuwa muongoza majadiliano hayo Dkt. Zakayo Lukumay.

Mratibu wa programu ya maboresho ya sekta ya sheria Bw. Emmanuel Mayeji akichangia mada.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Bi. Anne Malipula akichangia mada.

Wadau mbalimbali wakifuatilia majadiliano.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Wizara ya Katiba na Sheria yajipanga kwa maboresho ya sekta ya sheria awamu ya pili kwa kujadili taarifa ya utafiti wa kuhakiki visababishi vya changamoto zinazoikabili sekta ya sheria nchini.

Majadiliano hayo ya siku moja  yamefanyika jijini Morogoro miongoni mwa wadau wa sekta ya sheria wakati wakijiandaa kuandika andiko la pili la kutekeleza programu ya maboresho ya sekta ya sheria.

Mratibu wa Programu hiyo Bw. Emmanuel Mayeji amesema katika awamu ya kwanza ya kutekeleza programu ya maboresho ya sekta ya sheria mafanikio makubwa yalipatikana na uboreshaji ulionekana katika upande wa mahakama, Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo, Polisi na Magerezani.

"Mafanikio makubwa yamepatikana katika awamu ya kwanza ya uboreshaji hasa upande wa Mahakama, polisi , magereza na taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania" alisema.

Aliongeza, Kabla ya kuanza kutekelezwa kwa andiko la awamu ya pili ya programu hiyo Serikali iliielekeza Wizara ya Katiba na Sheria kuainisha changamoto zilizojitokeza katika awamu ya kwanza ili ziweze kutatuliwa kabla ya kuanza kwa awamu ya pili.

Programu ya Maboresho ya sekta ya sheria awamu ya kwanza ilifanikiwa kujenga majengo mbalimbali ya mahakama, ofisi na nyumba za watumishi, kununua vitendea kazi na kutoa mafunzo kwa watumishi mbalimbali waliopo katika sekta ya sheria hii yote ni katika kuifanya sekta hii kufanya kazi zake ipasavyo na kutoa haki kwa wakati.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA