MAZUNGUMZO YA AMANI YATAJWA KUWA NJIA BORA NA SALAMA YA UTATUZI WA MIGOGORO NCHINI.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Mazungumzo ya amani ni muarobaini uliothibitika kutumika kama tiba ya migogoro ya ardhi Mvomero Mkoani Morogoro. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Albinus Mgonya wakati akitoa taarifa ya hali ya amani wilayani humo kwa Kamati ya Kitaifa ya Ujenzi wa Amani na Kuzuia Mauaji ya Kimbari iliyofika walayani kwake hivi karibuni. Wakulima na wafugaji ni watanzania wanaoishi pamoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi katika maeneo wanaoishi na zaidi, wengi wao ni wakulima na ni wafugaji kwa wakati mmoja hivyo njia ya mazungumzo ya amani imejipambanua kuwa tiba ya utatuzi wa migogoro inayowakabili. "Unajua, hawa wakulima na wafugaji wanafahamiana kwasababu wanaishi pamoja, matumizi ya nguvu hususani vyombo vya ulinzi na usalama isingekuwa muarobaini, badala yake kwa kuwakutanisha na kuzungumza nao kumeonesha kuwa ni suluhisho la migogoro na ujenzi wa amani na utul...