PROF. MCHOME ATAKA WATANZANIA KUTUMIA VIZURI RASILIMALI ZILIZOPO NCHINI ILI KUJILETEA MAENDELEO
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akifungua kikao cha Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi cha kujadili Mfumo Jumuishi wa Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Rasilimali za Nchi kilichofanyika jijini Arusha.
Nchi ya Tanzania imebarikiwa
utajiri wa asili na rasilimali asilia ambazo zikitumika ipasavyo nchi na
wananchi wake watakuwa na maendeleo ya kiuchumi.
Profesa Mchome alisema Sheria ya
Usimamizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia ilitungwa ili kuweza kusaidia
kulinda rasilimali zilizopo nchini ili ziweze kuwanufaisha wananchi wake.
Alisema “Utajiri wa Asili na Maliasilia
zinatakiwa zitumike kwa manufaa ya nchi na watu wake na sio kwa manufaa ya nchi
za nje, mwaka 2017 tulitunga sheria ambayo ilisaidia kuweka miongozo jinsi gani
tuenende katika eneo hilo na jinsi gani watu watafaidi kutokana na maliasilia zao na utajiri ambao upo katika nchi yao”.
Alisema, Wawekezaji wadogo
wameanza kuongezeka na kufanya shughuli za uzalishaji kwa vibali halali na kwa
uhuru bila kukimbizwakimbizwa na hivyo kuongeza pato la nchi.
Profesa Mchome alisisitiza, kwa
sasa ardhi inatumika vizuri haitumiki kwa mtu mmoja kushika eneo kubwa bila
manufaa yoyote kwa wananchi sasa ardhi inatumika na kuwapatia wananchi manufaa
ambayo wanahitaji katika makazi, kilimo na maeneo mengine kwa hiyo malalamiko
yameanza kupungua na wananchi wameanza kuwa wamiliki wa ardhi ambao ni utajiri
wa asili na mali asilia unaozungumziwa.
Katibu Mkuu wizara ya katiba na
sheria ,Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa,endapo nchi yetu itazitumia
rasilimali tulizonazo itasaidia sana kuharakisha shughuli za maendeleo Kama
zilivyo kwa nchi zingine ambazo uchumi wao umeweza kukua kutokana na matumizi
mazuri ya rasilimali hizo.
Aidha, Mhadhiri Mwandamizi wa
Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Saalam (UDSM),Dokta Abel Kinyondo alisema
kuwa,Kuna njia mbili za kuhakikisha wananchi wananufaika na Kodi na tozo
mbalimbali zinazotokana na maliasili zetu serikali inazitumia kwa namna ya kimkakati
kuwarudishia wale walioko chini kabisa waweze kunufaika nazo.
Dokta Kinyondo alisema kuwa
,lazima tujue kuwa kwenye kufaidika zaidi na kwenye hela zaidi sio kwenye tozo
na Kodi bali wananchi waunganishwe moja kwa moja katika mnyororo wa thamani katika
maliasili kwani sehemu kubwa ya mapato inatokana na rasilimali.
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkaazi
wa UNDP, Bi Christine Musisi ambao ndio wafadhili wa kikao hicho, alisema wapo
tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha rasilimali za nchi
zinalindwa na kunufaisha wananchi wake.
Comments
Post a Comment