MKUU WA MKOA WA TANGA ATAKA TAASISI ZA UTOAJI HAKI ZIBORESHWE ILI ZIWEZE KUTOA HAKI KWA WAKATI
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigella ataka taasisi za utoaji haki ziendelee kuboreshwa ili haki iweze kupatikana kwa wakati. Mhe. Shigella aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa kamati za usalama za mkoa na Wilaya, kamati za maadili ya Mahakimu na Kamati za Parole mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria. Mhe. Mkuu wa Mkoa aliwaambia viongozi hao kuwa wana dhamana kubwa ya kuhakikisha nchi ina utulivu, amani na usalama hivyo waitumie fursa hii ya kupata mafunzo hayo vizuri na kushirikishana na wengine. “Tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha utulivu, usalama na amani ya nchi tunaitimiza kwa Pamoja, tutumie fursa hii vizuri na tushirikishane” alisema Mhe. Shigella. Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema mamlaka za kutenda haki mkoani humo ikiwemo Mabaraza ya ardhi ya kata yamekuwa yakilalamikiwa sana kutokana na ufanisi wake ambao unasababishwa na watumishi wachache waliopo ambayo inasababisha ucheleweshwaji wa maj...