MKUU WA MKOA WA TANGA ATAKA TAASISI ZA UTOAJI HAKI ZIBORESHWE ILI ZIWEZE KUTOA HAKI KWA WAKATI
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Mhe. Martin Shigella ataka taasisi za utoaji haki ziendelee kuboreshwa ili haki
iweze kupatikana kwa wakati.
Mhe. Shigella aliyasema
hayo wakati akifungua mafunzo kwa kamati za usalama za mkoa na Wilaya, kamati
za maadili ya Mahakimu na Kamati za Parole mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria.
Mhe. Mkuu wa Mkoa
aliwaambia viongozi hao kuwa wana dhamana kubwa ya kuhakikisha nchi ina
utulivu, amani na usalama hivyo waitumie fursa hii ya kupata mafunzo hayo
vizuri na kushirikishana na wengine.
“Tuna dhamana kubwa ya
kuhakikisha utulivu, usalama na amani ya nchi tunaitimiza kwa Pamoja, tutumie
fursa hii vizuri na tushirikishane” alisema Mhe. Shigella.
Aidha, Mkuu wa Mkoa
amesema mamlaka za kutenda haki mkoani humo ikiwemo Mabaraza ya ardhi ya kata
yamekuwa yakilalamikiwa sana kutokana na ufanisi wake ambao unasababishwa na
watumishi wachache waliopo ambayo inasababisha ucheleweshwaji wa majukumu yao
ikiwemo kupatikana kwa nakala za hukumu.
Aliongeza, Mkoani Tanga
chama cha wanasheria kimeendelea kutoa msaada mkubwa sana wa kisheria kwa
wananchi lakini bado hautoshelezi kwani matatizo ya kisheria ni mengi hivyo
awaomba waendelee kujitangaza ili wananchi waweze kuwafahamu na kwenda kupata
msaada wa kisheria. Pia aliahidi ofisi za Wakuu wa Wilaya na Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa zipo tayari kusaidia gharama ndogondogo ambazo zitahitajika kuendesha kesi
za wananchi zinapoenda mahakamani.
“Msaada mnaotoa ni
ibada na sehemu ya sadaka kwani unagusa Maisha ya watu wengi tena wengine
kutoka mbali na mlipo hivyo mjitahidi kuwasikiliza na kuwasaidia” alisema
Mhe.Shigella.
Aidha, Mkuu wa Mkoa
alisema mafunzo haya yanayohusisha viongozi wengi wakiwemo mahakimu yamekuja
wakati muafaka na wakati serikali ya awamu ya tano muhula wa pili unapoanza
hivyo ana imani yatawasaidia katika kutekeleza majukumu yao.
Comments
Post a Comment