WAJUMBE WA MABARAZA YA ARDHI ACHENI KUPOKEA RUSHWA – MHE. NGUVIRA
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Mkuu wa Wilaya ya
Handeni Mkoani Tanga Mhe. Toba Nguvira awaasa wajumbe wa mabaraza ya ardhi
wilayani humo kuacha tabia ya kupokea rushwa na kunyima haki wananchi.
Mhe. Nguvira aliyasema
hayo wakati akifungua mafunzo ya utawala bora, Wosia na Mirathi kwa watendaji
kata na wenyeviti wa mabaraza ya ardhi wilayani humu ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria ambayo kitaifa yalizinduliwa tarehe
12 Mkoani Tanga.
Mkuu wa wilaya huyo
aliwaambia watendaji kata na wenyeviti wa mabaraza ya kata hao wayatumie
mafunzo hayo vizuri ili kumaliza migogoro mingi iliyopo ambayo inaanzia kwenye
kata na inasababishwa na rushwa na hivyo kunyima haki baadhi ya wananchi.
“Migogoro ya ardhi na
mirathi ni mingi sana nchini na inasababishwa na rushwa” alisema Mkuu wa wilaya
huyo.
Aidha Mhe. Nguvira
alisema sheria zimewekwa kuhakikisha haki inatendeke kwani kukosekana kwa haki
kunapelekea machafuko katika jamii.
Mhe. Nguvira
aliwasisitiza wajumbe wa mafunzo hayo kuyatendea haki kwa kuyatumia mafunzo
watakayopata kuyatafsiri katika mabaraza ya kata.
Aimshukuru Mkuu wa
Wilaya kwa nasaha zake kabla ya kuanza kw mafunzo mwezeshaji wa mafunzo hayo
amabye pia ni Naibu Katibu kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw.
Calist Luanda alisema amepewa jukumu la kiutoa mafunzo kwa wajumbe hao hivyo
awasisitiza wajumbe kuyafanyia kazi mafunzo watakayopewa ili waweze kuboresha
kazi zao na kutoia haki kwa wananchi.
Comments
Post a Comment