WATUMISHI WIZARA YA KATIBA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU UANGALIZI WA UTAJIRI WA ASILI NA MALIASILIA

Mkurugenzi Idara ya Huduma za Kisheria Bw. Griffin Mwakapeje akifungua mafunzo ya siku mbili ya kujengea uwezo watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika eneo la Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia za nchi katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma. Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo. Mtoa mada kutoka shirika la Petroli la Taifa (TPDC) Dkt. Elias akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo. Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo. XXXXXXXXXXXXXXX Kitengo cha Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia kimeandaa mafunzo ya siku mbili kwa watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya Uangalizi wa Utajiri na Maliasilia. Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria Bw. Griffin Mwakapeje ambapo alisema mwaka 2017 Serikali iliwasilisha Bungeni miswada ya kutunga sheria mbili za usimamizi wa maliasilia za nchi. Alisema, hatua za kutunga sheria hizi mbili zilipelekea kujenga uel...