WAZIRI MWIGULU APONGEZA UONGOZI WA MAHAKAMA KWA KUTOA USHIRIKIANO NA KUWAPA NGUVU TAWJA KUFANIKISHA KAZI ZAO
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Geofrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Mgeni rasmi-Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akikabidhiwa Tuzo na Mwenyekiti wa
Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake (TAWJA) Mhe Jaji Joaquuine
De-Mello kwa kutambua mchango wake kwa majaji na mahakimu wanawake mara
baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT)
Jijini Mwanza.
Jaji Mkuu
wa Tanzania, Mhe Prof. Ibrahim Hamis Juma akikabidhiwa Tuzo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake (TAWJA)
Mhe Jaji Joaquuine De-Mello ya kutambua mchango wake kwa Majaji na Mahakimu wananwake wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na
Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa
Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Serikali imefurahishwa kwa kazi zinazofanywa na Chama cha Majaji
na Mahakimu Wanawake TAWJA katika kupigania haki za wananchi.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba
akimuwakilisha Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akifungua Mkutano Mkuu
wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7
Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Amewataka majaji hao kuendelea kuongeza na kuimarisha Haki
za Wanawake katika suala la Haki Sawa kwa wote; Kukuza Upatikanaji wa Haki kwa
Wanawake, Kukuza/Kuendeleza Uongozi wa Mahakama; Kufanya tafiti za kisheria
katika Usawa wa Kijinsia na Haki za Binadamu; Kubadilishana taarifa katika
masuala tata yanayowahusu Wanawake na kuondoa Upendeleo wa Kijinsia na Ubaguzi
wa aina yeyote.
Amesema kuwa mtazamo mkubwa wa TAWJA ni kuhakikisha
Majaji Wanawake na Mahakimu pamoja na Maafisa wengine wa Mahakama na Washirika
wanaandaliwa kwa kuwapatia nyenzo sahihi na muhimu zinazohitajika katika kukuza
Haki Sawa kwa Wote (‘Equal Justice for All’)
“Ninafahamu kuwa mmekuwa mkifanya hivyo bila kuchoka kwa
kipindi cha miaka ishirini (20) mfululizo tokea TAWJA kuanzishwa kwake mwaka
2000. Kwa hili niwapongeze sana Wanachama wote, mnatakiwa kujivunia na kutembea
kifua mbele kwa kazi nzuri mnazofanya. Naamini kuwa hili lisingewezekana bila
msaada mkubwa kutoka kwa Mahakama ya Tanzania Bara na Zanzibar” Alikaririwa Dkt
Mwigulu
Dkt Mwigulu amesema ni wazi kuwa sauti zao Majaji
na Mahakimu Wanawake ikijumuisha na zile za Wadau wengine nchini zimepelekea
utayari, uwazi na hamasa katika kulaani ubaguzi na ukiukwaji wa Haki za
Binadamu unaofanywa na wanajamii katika maeneo yetu.
Waziri Mwigulu amesema kuwa kaulimbiu ya Mkutano
huo ni; “Weledi na Ustawi wa Majaji Na Mahakimu Wanawake: Chachu ya
Mabadiliko”, imekuja wakati muafaka na mahali sahihi kwani mara nyingi
Wanawake Wataalamu hawatilii maanani ustawi wao, na hasa Maafisa wa Mahakama
ambao muda wote hutingwa zaidi na majukumu yao ya msingi.
Kutokana na Kaulimbiu hiyo, mtaibua vitu vingine
vilivyojificha na vinayowakabili Maafisa wa Mahakama amesisitiza katika
mkutano huo kujadiliwa kwa kina kuhusu masuala yahusuyo afya za akili na
mwili na kudadavua kuhusu uchumi, masuala ya kisaikolojia sambamba na kuangalia
ukuaji katika maeneo ya utoaji haki.
“Maendeleo ya Mwanamke ni maendeleo ya wote. Hivyo ni lazima
kumpa mwanamke kipa umbele. Ni muhimu sana kumpa mwanamke nafasi nyingi bila
kujali kuwa ni haki yake ya msingi kwani pia ni kuonyesha matumizi mazuri ya
uelewa wa uchumi.” Amesisitiza
Comments
Post a Comment