Tuesday, March 30, 2021

WAZIRI NCHEMBA AWASILISHA MPANGO NA MAKADIRIO YA BAJETI YA WIZARA KWENYE KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA KWA MWAKA 2021/2022

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (kushoto) akiongea wakati akiwasilisha mpango na makadirio ya bajeti ya wizara kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2021/2022.Mwenye miwani nyeusi ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Amon Mpanju.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akifuatilia hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ya mpango na makadirio ya bajeti ya wizara kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2021/2022, mwingine pichani ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu  wa RITA Bi. Emmy Hudson.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Mohamed Mchengerwa akiongea wakati kamati hiyo ilipokuwa ikisikiliza hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ya mpango na makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia  hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) ya mpango na makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia  hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) ya mpango na makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Saturday, March 13, 2021

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YAKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA MKOA NJOMBE

Jengo la Mahakama ya Mkoa Njombe likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi.
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yakagua mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Mkoa Njombe  leo 13/3/2021.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akipata maelezo kuhusu ujenzi wa mradi wa Mahakama ya Mkoa Njombe.


Viongozi wa Wizara wakiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kukagua mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Mkoa Njombe  leo 13/3/2021.

ZIARA YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA KATIKA MAHAKAMA YA MWANZO KIBAIGWA


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea mahakama ya Mwanzo Kibaigwa.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiwa katika ziara ya kutembelea mahakama ya Mwanzo Kibaigwa.
 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (katikati) akibadilishana mawazo na Naibu waziri wa wizara hiyo Mhe. Geophrey Pinda (kushoto) na Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kutembelea mahakama ya Mwanzo Kibaigwa.

 
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiwa katika ziara ya kutembelea mahakama ya Mwanzo Kibaigwa.

Tuesday, March 9, 2021

WATUMISHI WANAWAKE WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Watumishi Wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakisherehekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.Watumishi Wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wakishiriki maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Watumishi Wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wakifuatilia hotuba mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.Friday, March 5, 2021

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAANZA ZOEZI LA KUTAFSIRI SHERIA ZOTE NCHINI KUWA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

Wataalamu kutoka taasisi za sheria ikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Kurekebisha Sheria na chama cha wanasheria Tanganyika wakiongozwa na Wanasheria wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea na zoezi la kutafsiri sheria kuwa katika lugha ya kiswahili. Awamu ya kwanza ya zoezi hili ilianza kufanyika Machi 3 na inategemea kukamilika Machi 11, 2021 na itahusisha utafsiri wa sheria 16. Kazi ya kutafsiri sheria zote itafanyika kwa awamu tatu ambapo awamu hizo zinategemea kukamilika mwezi Disemba, 2021.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Kikao kazi cha wataalamu wa sheria kutoka taasisi mbalimbali wakiongozwa na Wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria chaanza kazi ya kutafsiri sheria zote nchini.

Kikao kazi hicho cha awamu ya kwanza cha siku 8 kilichoanza kazi Machi 3 kinatarajiwa kukamilisha kazi yake Machi 11 kwa kutafsiri sheria 16.

Huu ni utekelezaji wa agizo lilitolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba  kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome Disemba 22, 2020 alipotembelea Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania. Katika ziara hiyo waziri Dkt. Nchemba alisema sheria ni sekta inayomsaidia mtu kupata haki hivyo inapaswa lugha ya Kiswahili itumike kwanza katika masuala mbalimbali ya kisheria kisha lugha nyingine ziwe ni za nyongeza, hivyo sheria, mwenendo wa mashauri na hukumu iandikwe kwa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha wananchi kuelewa kwa urahisi kuhusu kesi zao,

Zoezi hili la kutafsiri sheria linategemewa kufanyika kwa awamu tatu kabla ya kuhakikiwa kwa tafsiri hiyo kuangalia kama kilichotafsiriwa ni sahihi na hakijapoteza maana ya kile kilichokusudiwa katika utungwaji wa sheria husika.

Zoezi la kutafsiri sheria linatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2021 ambapo sheria zote nchini zinatarajiwa kuwa zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.


Tuesday, March 2, 2021

SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA PILI WA MABORESHO ENDELEVU YA HAKI MTOTO


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto hapa nchini uliofanyika Machi 2, 2021 jijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba akizindua mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto hapa nchini, uzinduzi huo umefanyika Machi 2, 2021 jijini Dodoma.Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto hapa nchini uliofanyika Machi 2, 2021 jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Griffin Mwakapeje akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto hapa nchini uliofanyika Machi 2, 2021 jijini Dodoma.Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba ( wa tatu kulia) akiwa na viongozi kutoka wizara mbalimbali wakionyesha nakala za mpango mkakati wa pili wa haki mtoto.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome kuhakikisha Mpango wa Pili wa Maboresho Endelevu ya Haki Mtoto nchini unatafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili ujumbe uifikie jamii kwa urahisi.

Waziri Nchemba ameyasema hayo wakati akizindua Mpango Mkakati wa Pili wa Haki Mtotoambapo alisema utumiaji wa lugha ya Kiswahili katika utekelezaji wa mpango huo utasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa kwani kila mmoja ataweza kuwajibika kwa nafasi yake kuleta ustawi wa mtoto nchini.

Alisema, Wizara itaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuratibu vyema mpango huo ikiwemo kuimarisha mfumo wa ulinzi wa mtoto, kuongeza uelewa wa haki za mtoto katika jamii, kufanyika kwa maboresho ya sera na sheria Pamoja na kuimarisha uratibu wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mkakati.

“Lengo la Serikali ni kumlinda mtoto apate haki zake za msingi lakini hili haliwezi kufikiwa ikiwa shughuli zetu tunazifanya kwa lugha za kigeni wakati walengwa ni watanzania , Katibu Mkuu hakikisha hili linafanyika kwa lugha ya Kiswahili tunataka wananchi wetu waelewe, tunatarajia mkakakti huu uwe na matokeo chanya kwa Watoto” alisema  Waziri Nchemba.

Vilevile, WaziriNchemba aliagiza kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo angalau mara nne kwa mwaka hatua itakayosaidia ufuatiliaji, tahthmini nah atua za kuchukua kuboresha pindi changamoto zinapojitkeza huku akiziagiza taasisi kubainisha majukumu yao kuelekea bajeti kuu ya Serikali.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika MpangoNkakati wa kwanza alisema uliwezesha uliwezesha kuboreshwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu mtoto ambapo moja ya sheria iliyorekebishwa ni ya dini inayosema kuingia katika mahusiano ya ndoa ni kosa la ubakaji.

“Nitoe rai kwa taasisi kujenga uelewa kwa jamii kuhusu haki na wajibu wao kwa mtoto, mwaka 2017 ilitungwa sheria ya msaada wa kisheria iliyosaidia Watoto katika masuala ya kisheria ikiwemo kuwakilishwa mahakamani, uanzishwaji wa madawati ya jinsia katika vituo vyote vya polisi, pamoja na kufanikiwa huku hatutaishia hapa tuna wajibu wa kuwalinda na kuwaandaa wawe raia wema katika taifa letu na wasimame wenyewe katika Maisha yao”, alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umojawa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Shalini Bahuguna aliipongezaSerikali kwa juhudi kubwa inazochukua kulinda haki za mtoto mijini na vijijini.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kushirikiana na Mashirika mbalimbali na tumeona juhudi zenu kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira salama na kupata haki zake, tunategemea Mpango Mkakakti huu utakuwa na manufaa na tuko tayari kushirikiana na nyinyi” alisema Mwakilishi Mkaazi huyo.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchomealieleza baadhi ya changamotowanazokabiliana nazo alisema ni Pamoja na uchache wa wataalamuwa masuala ya Watoto, taasisi kutotenga bajeti, baadhi ya magereza kukosa sehemu maalum kwa ajili ya Watoto.

“Harakati za kufanikisha usalama wa mtoto zinaendelea kwani maafisa 638 kutoka kanda 14 wanaoendesha kesi za Watoto walijengewa uwezo, huduma za msaada wa kisheria zimeongezeka, na mahakama za Watoto zimeongezeka kutoka moja hadi 130” alisema.

Aidha mmoja wa wadauwalioshiriki katika uzinduzi huo Bi. Fatma Abdalah ambaye ni Kamishna kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, alisema tume hiyo imeanzisha mfumo wa mtandao utakaosaidia wananchi kutoa malalamiko yao ili kuwafikia wengi Zaidi na kulinda utu wa mtoto.