SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA PILI WA MABORESHO ENDELEVU YA HAKI MTOTO


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto hapa nchini uliofanyika Machi 2, 2021 jijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba akizindua mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto hapa nchini, uzinduzi huo umefanyika Machi 2, 2021 jijini Dodoma.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto hapa nchini uliofanyika Machi 2, 2021 jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Griffin Mwakapeje akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa pili wa maboresho endelevu ya haki mtoto hapa nchini uliofanyika Machi 2, 2021 jijini Dodoma.



Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba ( wa tatu kulia) akiwa na viongozi kutoka wizara mbalimbali wakionyesha nakala za mpango mkakati wa pili wa haki mtoto.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome kuhakikisha Mpango wa Pili wa Maboresho Endelevu ya Haki Mtoto nchini unatafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili ujumbe uifikie jamii kwa urahisi.

Waziri Nchemba ameyasema hayo wakati akizindua Mpango Mkakati wa Pili wa Haki Mtotoambapo alisema utumiaji wa lugha ya Kiswahili katika utekelezaji wa mpango huo utasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa kwani kila mmoja ataweza kuwajibika kwa nafasi yake kuleta ustawi wa mtoto nchini.

Alisema, Wizara itaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuratibu vyema mpango huo ikiwemo kuimarisha mfumo wa ulinzi wa mtoto, kuongeza uelewa wa haki za mtoto katika jamii, kufanyika kwa maboresho ya sera na sheria Pamoja na kuimarisha uratibu wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mkakati.

“Lengo la Serikali ni kumlinda mtoto apate haki zake za msingi lakini hili haliwezi kufikiwa ikiwa shughuli zetu tunazifanya kwa lugha za kigeni wakati walengwa ni watanzania , Katibu Mkuu hakikisha hili linafanyika kwa lugha ya Kiswahili tunataka wananchi wetu waelewe, tunatarajia mkakakti huu uwe na matokeo chanya kwa Watoto” alisema  Waziri Nchemba.

Vilevile, WaziriNchemba aliagiza kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo angalau mara nne kwa mwaka hatua itakayosaidia ufuatiliaji, tahthmini nah atua za kuchukua kuboresha pindi changamoto zinapojitkeza huku akiziagiza taasisi kubainisha majukumu yao kuelekea bajeti kuu ya Serikali.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika MpangoNkakati wa kwanza alisema uliwezesha uliwezesha kuboreshwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu mtoto ambapo moja ya sheria iliyorekebishwa ni ya dini inayosema kuingia katika mahusiano ya ndoa ni kosa la ubakaji.

“Nitoe rai kwa taasisi kujenga uelewa kwa jamii kuhusu haki na wajibu wao kwa mtoto, mwaka 2017 ilitungwa sheria ya msaada wa kisheria iliyosaidia Watoto katika masuala ya kisheria ikiwemo kuwakilishwa mahakamani, uanzishwaji wa madawati ya jinsia katika vituo vyote vya polisi, pamoja na kufanikiwa huku hatutaishia hapa tuna wajibu wa kuwalinda na kuwaandaa wawe raia wema katika taifa letu na wasimame wenyewe katika Maisha yao”, alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umojawa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Shalini Bahuguna aliipongezaSerikali kwa juhudi kubwa inazochukua kulinda haki za mtoto mijini na vijijini.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kushirikiana na Mashirika mbalimbali na tumeona juhudi zenu kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira salama na kupata haki zake, tunategemea Mpango Mkakakti huu utakuwa na manufaa na tuko tayari kushirikiana na nyinyi” alisema Mwakilishi Mkaazi huyo.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchomealieleza baadhi ya changamotowanazokabiliana nazo alisema ni Pamoja na uchache wa wataalamuwa masuala ya Watoto, taasisi kutotenga bajeti, baadhi ya magereza kukosa sehemu maalum kwa ajili ya Watoto.

“Harakati za kufanikisha usalama wa mtoto zinaendelea kwani maafisa 638 kutoka kanda 14 wanaoendesha kesi za Watoto walijengewa uwezo, huduma za msaada wa kisheria zimeongezeka, na mahakama za Watoto zimeongezeka kutoka moja hadi 130” alisema.

Aidha mmoja wa wadauwalioshiriki katika uzinduzi huo Bi. Fatma Abdalah ambaye ni Kamishna kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, alisema tume hiyo imeanzisha mfumo wa mtandao utakaosaidia wananchi kutoa malalamiko yao ili kuwafikia wengi Zaidi na kulinda utu wa mtoto.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA