Friday, April 23, 2021

MHE. PROF. KABUDI AKUTANA NA MWAKILISHI MKAAZI WA UN WOMEN

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN Women) Hodan Addouh alipomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma. 
 
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akifanya mazungumzo na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN Women) Hodan Addouh (wa pili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma. 

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN Women) Hodan Addouh (wa pili kulia) alipomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma.

Miongoni mwa mambo waliyojadiliana Waziri Kabudi na mgeni wake ni pamoja na shirika hilo kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Katiba na Sheria katika masuala ya utoaji msaada wa kisheria, mimba za utotoni na ndoa katika umri mdogo.

Na Waziri Kabudi ameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha na kushirikiana na Wizara na Taasisi nyingine katika yale yote yatakayohitajika ambayo Shirika hilo linayaunga mkono.


Thursday, April 22, 2021

KAMISHENI YA AFRIKA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAIPONGEZA TANZANIA KWA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO

 


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof.Palamagamba Kabudi,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada ya kumaliza kuwasilisha ripoti ya haki za binadamu katika kikao cha 68 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za binadamu na Watu uliofanyika kwa njia ya Mtandao.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Tanzania imewasilisha ripoti ya haki za binadamu kwenye kikao cha 68 cha Kamisheni ya Afrika ya haki za binadamu na watu, huku kamisheni hiyo ikiipongeza kwa kupiga hatua kubwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi hasa suala la kusambaza umeme vijijini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao kikijumuisha nchi zote wanachama na makao Makuu ya kamisheni ambayo ni nchi ya Gambia, Waziri wa Katiba na sheria Prof. Palamagamba Kabudi,amesema kuwa mara baada ya mawasilisho hayo Kamisheni imeipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika miradi ya maendeleo ambayo inagusa wananchi moja kwa moja katika kujiletea maendeleo.

“Moja wameridhika kwa kiasi kikubwa sana katika miradi ya maendeleo, ambapo mwenyekiti amerudia tena kupongeza katika suala la kusambaza umeme vijijini ambapo kwa miaka mitano tumefikisha vijiji 9112 vilivyopata umeme kutoka vijiji 2114 mwaka 2015, kati ya vijiji vilivyopo 12268 katika nchi yetu” amesema Prof.Kabudi.

Aidh amesema katika ripoti waliyoiwasilisha wameonyesha mambo makubwa yaliyofanyika ndani ya nchi ya Tanzania kuhusu haki za binadamu ambayo yanaunganisha haki za kisiasa, uchumi, kijamii, na kiutamaduni ambapo Tanzania imepiga hatua katika elimu na afya na huduma nyingine za kijamii kama maji safi hasa maeneo ya vijijini.

“Katika sekta ya elimu tumeeleza hatua kubwa tuliyoipiga hasa kwa kutekeleza elimu bila malipo ambapo kila mwezi tumekuwa tukitoa shilingi bilioni 24 katika kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure na katika afya ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, Zahanati na hospitali za rufaa za Mikoa ” amesema.

Suala lingine ni Kiswahili kuwa lugha rasmi ya mahakama katika kuandika sheria na kutoa hukumu na kazi mbalimbali za Mahakama, pia Tanzania kuwa nchi ya kwanza kwa Afrika Mashariki kutoa msaada wa huduma za kisheria kwa makosa ya kijinai na masuluhishi mbalimbali.

“Katika hili hivi sasa kila Halmashauri ya Wilaya hapa nchini wanae msajili msaidizi wa haki za binadamu ambapo kwa sasa tunawasajili 209 kwa Tanzania nzima katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kisheria” Prof.Kabudi

Kuhusu haki ya kupata habari amesema katika ripoti hiyo wameonyesha kuwa mpaka hivi sasa wananchi wanapata habari za kila aina kutoka vyombo mbalimbali ambapo Magazeti ni 250, Televisioni 44, Radio 198, Online Televisioni 440, Online Radio 23, na Blog 120, vyombo vyote hivi vikitoa habari za aina mbalimbali.

Ameongeza kuwa “Pia tumeeleza idadi ya wanawake katika vyombo vya maamuzi, ambapo kwa sasa tuna Rais Mwanamke, Naibu Spika mwanamke, vile vile katika Bunge asilimia 36 ni wanawake, katika ngazi za Mahakama za rufaa asilimia 44 ni wanawake, Mahakama kuu asilimia 33, mahakama za hakimu mkazi asilimia 50, asilimia 42.5 katika mahakama za mwanzo na asilimia 40 katika nafasi za wasajili wa mahakama” amesema.

Prof.Kabudi amesema kuwa mambo yote yametekelezwa ikiwa ni katika kuhakikisha haki katika makundi mbalimbali zinapatikana hasa katika kupata huduma za kijamii kwa wananchi wa Tanzania.

 

Wednesday, April 21, 2021

Mhe. GEOPHREY PINDA AONGOZA KIKAO CHA WAKUU WA TAASISI KUPITIA HOTUBA YA BAJETI YA 2021/2022


 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda (kushoto) akiongoza kikao cha Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara kupitia hotuba ya bajeti ya wizara ya mwaka wa fedha 2021/2022.


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akiongoza kikao cha Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara kupitia hotuba ya bajeti ya wizara ya mwaka wa fedha 2021/2022.

Thursday, April 15, 2021

WAZIRI KABUDI AWATAKA WATUMISHI KUWA WAZALENDO WA NCHI YAO

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria.


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongea katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo. 


Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akifafanua jambo katika mkutano wa  Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo. 


Picha ya pamoja ya Waziri Kabudi na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi.
 

WAZIRI NCHEMBA AKABIDHI OFISI KWA WAZIRI KABUDI


 Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akimkabidhi nyaraka mbalimbali Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi ofisi baada ya Mhe. Kabudi kuteuliwa kuiongoza wizara hii.

Tuesday, April 13, 2021

WAZIRI KABUDI APOKELEWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi alipowasili wizarani hapo na kupokelewa na viongozi na watumishi wa wizara hiyo mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo baada ya mabadilikio madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Kabudi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome.Waziri Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria.

 
Waziri Kabudi (wa pili kulia) akisaini kitabu cha wageni alipoingia ofisini kwake.