KILA MTANZANIA ANA HAKI YA KUPATA TAARIFA – WAZIRI KABUDI


 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, akizungumza na wawakilishi wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa katika kikao  kilichofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa Bw. Kajubi Mukajanga akizungumza kwenye kikao chao na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, (hayupo pichani) wakati akizungumza na wawakilishi wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.


XXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi,amewataka watanzania na vyama visivyo vya kiserikali kulinda haki za binadamu na kufuata sheria za uhuru wa kujieleza  kwani ni jukumu  lao  kikatiba.

Pia amesema kuwa jukumu la serikali  ni kuhakikisha inasimamia na kuzilinda sheria hizo kupitia taasisi ya tume ya haki za binadamu na utawala bora.

Waziri.Kabudi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wawakilishi wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa.

Amesema katika kuhakikisha kila Mwananchi anakuwa na uhuru wa kupata habari serikali imeridhia mkataba wa Afrika wa mwaka1981 ambapo ibara ya 9 inaeleza kwamba kila mtu ana haki ya kupata taarifa na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake.

“Tanzania iliridhia mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za kiraia na kisiasa wa mwaka 1966 na juni 1976 ambapo ibara ya 19(1) inaeleza kuwa kila mtu anahaki kuwa na maoni yake bila kuingiliwa, kila mtu ana haki ya kujieleza ikijumuisha na kuomba na kupata habari.

Prof..Kabudi amezihakikishia  asasi zisizo za kiraia na  mashirika yanayosimamia Uhuru wa kujieleza  na haki ya kupata taarifa kama utekelezaji wa ibara ya 18 ya katiba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa Bw. Kajubi Mukajanga amesema kuwa sheria ya ATI ilipitishwa na kutiwa saini na Hayati Rais John Magufuli Septemba 23, 2016.

Amesema Malengo ya sheria hii ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa kuainisha wigo wa taarifa ambazo umma una haki ya kuzipata kukuza uwazi na uwajibikaji wa wenye taarifa; na kuainisha mambo mengine yahusianayo na hayo.

“Sheria hii inatoa uhai kwa haki ya kikatiba ya kupata taarifa, na inaeleza taratibu za kutumiwa na wananchi kupata taarifa, huku ikiweka shuruti kwa maafisa wa serikali na taasisi zinazotumia rasilimali fedha ya umma kutoa taarifa muhimu kwa wananchi bila kusubiri kuombwa.

“Lakini pamoja na nia hii njema, uhalisia ni kwamba utekelezaji wa sheria umekuwa ukisuasua na upatikanaji wa taarifa kwa wananchi haujaimarishwa kama inavyokusudiwa na sheria” amesema

Tafiti zilizofanywa na taasisi za Twaweza (2017) MCT (2019) pamoja na MISA-Tan (2020) zilibainisha kwamba raia wengi hawana ufahamu wa sheria hii, japo wanakubali kwamba taarifa zinazoshikiliwa na serikali ni rasilimali ya umma, amesema Mwenyekiti huyo.

 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA