PROF. MCHOME AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WAKATI WA KUJADILI MAPENDEKEZO YA KUANDAA SERA YA TAIFA YA MASHTAKA

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi zinazosimamia haki jinai na Wataalam kujadili mapendekezo ya kuandaa Sera ya Taifa ya Mashtaka.


Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Haki Jinai wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome wakati akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi zinazosimamia haki jinai na Wataalam kujadili mapendekezo ya kuandaa Sera ya Taifa ya Mashtaka.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi zinazosimamia haki jinai na Wataalam  wakati wa kujadili mapendekezo ya kuandaa Sera ya Taifa ya Mashtaka.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam  wakati wa kujadili mapendekezo ya kuandaa Sera ya Taifa ya Mashtaka.

                                             XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

SERA YA TAIFA YA MASHTAKA YATARAJIWA KUKAMILIKA DISEMBA 2021- PROF. MCHOME

Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara za Maliasili na Utalii, Mambo ya Ndani, TAMISEMI na Taasisi za TAKUKURU, Polisi, Magereza, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Uhamiaji zashirikiana kuandaa Sera ya Taifa ya Mashtaka.

Katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema Sera hiyo inategemewa kukamilika ifikapo Disemba 2021.

Profesa Mchome ameyasema hayo katika kikao kilichojumuisha Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Haki Jinai ikiwemo Makatibu Wakuu wa Maliasili na Utalii, Mambo ya Ndani, TAMISEMI, Wakuu wa Taasisi ikiwemo Jeshi la Magereza, Polisi, Takukuru, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Uhamiaji.

Amesema “Sisi kama Makatibu Wakuu tumeazimia kazi hii iendelee na ikamilishwe ifikapo Disemba 2021 ili kutupa muelekeo katika mambo mbalimbali ambayo tunayafanya katika tasnia ya utoaji haki lakini katika tasnia ya haki jinai na haswa katika eneo hili la uendeshaji wa mashtaka”.

Prof. Mchome ameongeza kuwa “Tumekutana Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi ambao tunahusika katika mfumo huo ili kuwasikiliza wataalam wetu wanatushauri nini katika mambo mbalimbali na tumeweza kupata maoni na yameweza kutusaidia ili tuweze kupata hali halisi ya mustakabali mzima wa haki jinai katika nchi yetu”.

Mbali na hayo alisema “Sekta ya sheria imekutana ili kuona namna gani tunatengeneza sera yetu itakayokuwa inagusa mfumo wa haki jinai kwa sababu nchi inaongozwa na katiba na sera na sheria ili kuona namna gani tunajenga huu mfumo ili kuona tuwezaje kuifikisha nchi yetu katika ulimwengu ambao tunauhitaji wenye uchumi ambao umeendelea kukua na kuona wananchi wameendelea kustawika katika mustakabali mzima wa taifa letu”.

“Tuliyoyaona ni mambo ambayo yanalenga zaidi katika kuimarisha mifumo yetu. Nchi yetu imepiga hatua tumepata vyombo vingi na vyenye kutenda kazi kwa namna ambayo nchi yetu imeendelea kuwa na amani na utulivu ambao tunao”.amesema

Kwa upande wao Manaibu Katibu Wakuu kutoka Mambo ya Ndani, TAMISEMI na Maliasili na Utalii wamesema pindi sera hiyo itakapokuwa tayari itawasaidia watendaji hao hasa katika upande wa sheria, kupatikana kwa haki na kuleta utofauti katika njia mablimbali zitakazotumika kujua au kuainisha matatizo yanayojitokeza katika jamii na maeneo husika katika utoaji huduma kupitia sekta hiyo.

Aidha, Lengo la kikao hicho ni kujadili maoni ya kuandaa Sera ya Mashtaka ya kuleta majawabu katika uimarishaji na uendeshaji wa kesi Jinai.

 

Vilevile, Katika kikao hicho maeneo 16 ya mapendekezo ya maoni yameainishwa ikiwemo mikakati miwili na tamko moja la kisera ili kuepukana na changamoto ya ucheleweshwaji wa haki kwa mwananchi, kuimarisha na kupunguza mzigo wa kazi kwa magereza pamoja na jeshi la polisi.

 



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA