TANZANIA SIO NCHI YA KWANZA KUTUMIA KISWAHILI KATIKA UTOAJI HAKI - PINDA

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Gephrey Pinda akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa  Mkutano wa kujadili matumizi ya kiswahili katika Tasnia ya sheria uliofanyika Juni 11,2021 jijini Dodoma.




Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju akitoa mada kuhusu mabadiliko ya sheria na hatua zilizochukuliwa na Serikali wakati wa Mkutano wa kujadili matumizi ya kiswahili katika Tasnia ya sheria uliofanyika Juni 11,2021 jijini Dodoma.



Mwalimu kutoka Shule kuu ya Sheria ya chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt. Asina Omari akitoa mada kwa washiriki wakati wa Mkutano wa kujadili matumizi ya kiswahili katika Tasnia ya sheria uliofanyika Juni 11,2021 jijini Dodoma.


Mratibu wa Mkutano wa kujadili matumizi ya kiswahili katika Tasnia ya sheria Dkt.Ayubu Rioba akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa kujadili matumizi ya kiswahili katika Tasnia ya sheria uliofanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geophrey Pinda akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya washiriki wakati wa  Mkutano wa kujadili matumizi ya kiswahili katika Tasnia ya sheria uliofanyika jijini Dodoma.




Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geophrey Pinda,(hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa kujadili matumizi ya kiswahili katika Tasnia ya sheria uliofanyika jijini Dodoma.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Tanzania siyo nchi ya kwanza kuacha lugha ya kigeni na badala yake kutumia lugha yake ya kiswahili katika utoaji wa haki kwa wananchi.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda wakati akifungua  Mkutano wa kujadili matumizi ya kiswahili katika Tasnia ya sheria. Waziri Pinda amewataka  washiriki kujadili kwa kina mchango wa Kiswahili nchini.

Mhe.Pinda amesema kuwa kuna nchi nyingine ambazo zimekuwa zikitumia lugha zao rasmi katika kutoa haki ikiwemo India na zimekuwa zikifanya vizuri katika eneo hilo

“Ziko nchi wanatumia lugha zao katika uandishi wa sheria na utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za haki, ifahamike kuwa asili ya lugha ya kisheria si kiingereza kama inavyofahamika na wengi bali lugha za kijerumani, kilatini na kifaransa kwa kuwa walionekana kustaarabika’’amesema Pinda

Hata hivyo amesema kuwa  licha ya lugha ya Kiswahili kuwa moja ya nguzo inayosimamia ukuaji wa uchumi,  serikali iliona umuhimu wa kuanza kutumia lugha hiyo katika utoaji na upatikanaji wa haki nchini.

”Kuna sheria nyingi ziko kwa kiingereza ambayo ineonekana kuwa ni changamoto katika upatikanaji wa haki nchini”amefafanua

Aidha Mhe.Pinda amewataka  wanasheria kujikita na kutumia lugha ya Kiswahili katika utoaji wa haki nchini.

‘’Niwaombe wanasheria kutumia lugha ya Kiswahili kuna watu wamekosa haki zao sababu hawafahamu lugha , ni wakati sasa kwa watanzania kutumia lugha yetu, hatuwezi kutumia lugha ambazo si za kwetu’’amesisitiza

Pinda amesema Kiswahili ni lugha ya kimataifa ikiwa ya kumi duniani yenye wazungumzaji wengi Barani Afrika na duniani kote.

Pia ameeleza kuwa Wizara inaratibu ukuzwaji na uendelezaji wa matumizi ya lugha ya kiswahili katika utoaji haki, kuratibu wasimamiaji haki katika sekta nyingine katika kutekeleza na kutoa haki nchini.

‘’Wizara ya katiba na sheria inaratibu zoezi la kutafsiri sheria zote kwa lugha ya Kiswahili, mchakato wa kutafsiri unafanywa ndani ya Wizara pamoja na taasisi zake’’ amesema Mhe. Pinda

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Amon Mpanju amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mfumo wa utoaji haki.

‘’Tumeona tukutane na wadau wenye ubobezi wa lugha hii ya Kiswahili ili tuje na misamiati itakayokubalika katika mfumo wa utoaji haki lakini pia tunahakikisha tunapata lugha sahihi ya Kiswahili tutakayoitumia katika mfumo wetu wa utoaji haki’’amesema Mpanju

Naye  Mwalimu kutoka Shule kuu ya Sheria ya chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt. Asina Omari akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki amesema kuwa watahakikisha kuwa wanakuwa na sheria ambazo zitasaidia wananchi kupata haki zao.

‘’Tumepokea maekezo tutakwenda kuyafanyia kazi ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki zao kupitia sheria’’amesema Dkt. Asina.

Mnamo tarehe 24/1/2021 Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alihudhuria ufunguzi wa Maadhimisho ya wiki ya sheria, alisisitiza kuwa ni vyema sheria za uendeshaji wa kesi mahakamani ikawa kwa lugha ya kiswahili.

Ikumbukwe kuwa Hayati Dkt John Pombe Magufuli wakati wa uhai wake alijipambanua katika matumizi ya lugha ya Kiswahili ambapo hotuba zake nyingi alizitoa kwa Kiswahili ambapo alihimiza umuhimu wa Kiswahili katika mfumo wa sheria na utoaji haki nchini katika nyakati tofauti.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA