WAZIRI KABUDI AAHIDI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WANANCHI KUFIKIA VYOMBO VYA HAKI

 

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wizara na viongozi wa shirika la mtandao wa watetezi wa haki za binadamu walipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongea na viongozi wa shirika la mtandao wa watetezi wa haki za binadamu walipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa  shirika la mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Bw. Onesmo Ngurumo akiongea wakati alipomtembelea Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi  ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa kutetea Haki za binadamu ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kama ilivyo ainishwa katika katiba na ilani ya Chama cha Mapindizi (CCM) 2020/2025.

 

Akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Kutetea Mashirika yanayotetea haki za Binadamu (THRDC) Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wa kutetea haki za binadamu kwenye masuala ya kupigania haki za msingi.

 

“Tuko tayari kushirikiana na wadau ninyi muhimu kwenye masuala ya kupigania haki za wananchi tunajua kuwa mtakua na vipaumbele vyenu muhimu na serikali pia itakuwa na vipengele vyake ambavyo vinalenga kukuza haki za binadamu nakuleta maendeleo katika nchi yetu.

 

“Hayo yote ni matakwa ya ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kuwa serikali imeahidi kuheshimu na kuzingatia haki za binadamu kwa mtu mmoja mmoja, makundi na makundi ili kujenga jamii yenye usawa,” alieleza kabudi.

 

Aidha alisema Tanzania sio nchi yakufundishwa kupigania haki za binadamu kwani ni suala ambalo lilianza tangu zamani sana na kila kitu kimeandikwa kwenye katiba.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mtandao wa THRDC Bw. Onesmo Olengurumwa alisema serikali inatambua kuwa mfumo bora wa sheria ndio msingi wa kutekeleza matakwa ya katiba, Sera, na mpango wa nchi.

 

Alisema asasi za kutetea haki za binadamu zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati.

“Asasi za kiraia zimekuwa zikifanya vizuri sana hapa nchini tunaomba serikali itambue mchango wa asasi hizo na kuongeza ushirikiano ili ziendelee kufanya vizuri kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla,” alisema.

 

Olengurumwa aliihakikishia serikali kuwa mashirika ya kutetea haki za binadamu yataendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati bila vipingamizi vyovyote.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA