Posts

Showing posts from October, 2021

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YANYAKUA MEDALI YA SHABA KWENYE MBIO ZA WAZEE

Image
  Bi.Georgina Mukwenda kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ameibuka mshindi wa pili(2) wa mbio za jumla za wazee na kuibuka na medali ya Shaba kwenye mashindano ya Shimiwi Mkoani Morogoro: Tunampongeza sana kwa kuiletea Wizara yetu ya Katiba na Sheria heshima kwenye mbio hizo zilizokuwa na ushindani mkali.

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YATINGA 16 BORA MICHUANO YA SHIMIWI

Image
Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Katiba na Sheria   imefanikiwa kuingia hatua ya kumi na sita bora mara baada ya kuisambaratisha   timu ya TARURA asubuhi ya leo kwa jumla ya goli 4 kwa bila kwenye michuano ya SHIMIWI   inayoendelea mkoani Morogoro. Aidha, timu ya kuvuta kamba ya Wanawake   nayo imeingia   hatua ya kumi na sita bora huku timu ya mpira wa pete ikisubiri hatma yake kwenye mchezo uliobaki. Ikumbukwe kuwa timu za Sheria zilikuwa kwenye makundi yenye timu nyingi Hivyo mchujo wake unapitia hatua za kumi na sita bora tofauti na makundi mengine ambayo yapo hatua ya robo fainali. Pichani juu kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Katiba na Sheria kilichoisambaratisha TARURA asubuhi ya leo kwa jumla ya goli 4-0. Pichani juu wachezaji wa  Katiba na Sheria wakipata mawaidha ya kocha kipindi cha mapumziko baada ya dakika 45 za mchezo dhidi ya  TARURA. Pichani juu makamu Mwenyekiti na Katibu wa SheriaSports Club pamoja na Kocha wa wa timu ya mpira wa miguu wakiteta jambo kabla ya m