WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YATINGA 16 BORA MICHUANO YA SHIMIWI


Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Katiba na Sheria  imefanikiwa kuingia hatua ya kumi na sita bora mara baada ya kuisambaratisha  timu ya TARURA asubuhi ya leo kwa jumla ya goli 4 kwa bila kwenye michuano ya SHIMIWI  inayoendelea mkoani Morogoro. Aidha, timu ya kuvuta kamba ya Wanawake  nayo imeingia  hatua ya kumi na sita bora huku timu ya mpira wa pete ikisubiri hatma yake kwenye mchezo uliobaki. Ikumbukwe kuwa timu za Sheria zilikuwa kwenye makundi yenye timu nyingi Hivyo mchujo wake unapitia hatua za kumi na sita bora tofauti na makundi mengine ambayo yapo hatua ya robo fainali.



Pichani juu kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Katiba na Sheria kilichoisambaratisha TARURA asubuhi ya leo kwa jumla ya goli 4-0.







Pichani juu wachezaji wa  Katiba na Sheria wakipata mawaidha ya kocha kipindi cha mapumziko baada ya dakika 45 za mchezo dhidi ya  TARURA.




Pichani juu makamu Mwenyekiti na Katibu wa SheriaSports Club pamoja na Kocha wa wa timu ya mpira wa miguu wakiteta jambo kabla ya mechi.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA