Posts

Showing posts from November, 2021

MKUTANO WA 58 WA SHIRIKA LA MASHIRIKIANO YA KISHERIA WA AFRIKA NA ASIA WAANZA MJINI HONGKONG CHINA.

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda, amemwakilishaWaziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ambaye ni Rais wa Mkutano wa 58 wa Shirika la Mashirikiano ya Kisheria wa Afrika na Asia (AALCO) katika mkutano huo unaofanyika HongKong China kuanzia tarehe 29 Novemba hadi 01 Disemba. Katika mkutano huo Mhe. Pinda aewasilisha hotuba ya Rais wa Shirika hilo. Aidha katika mkutano huo Prof. Gaston Kennedy ambaye ni Katibu Mkuu wa AALCO ameendesha mkutano huo wenye lengo la kumpata Katibu Mkuu mpya  baada ya Pro. Kennedy kumaliza muda wake.

CHETI CHA KUZALIWA NI HAKI YA MTOTO RAIA NA ASIYE RAIA – WAZIRI KABUDI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiongea katika hafla ya uzinduzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Katavi na Rukwa. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashatu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi. Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizindua mpango wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Katavi na Rukwa. Waziri Kabudi akitoa vyeti vya kuzaliwa watoto kwa wazazi waliofika katika viwanja vya shule ya msingi Kashatu Mkoani Katavi kusajili watoto wao. Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya ambaye alikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria kwenye hafla hiyo akitoa salamu za wizara. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila mtoto aliyezaliwa Tanzania awe raia au asiwe raia, hii itasaidia utambuzi wa wananchi na kuwezesha Serikali kupanga mipango ya maendeleo ipasavyo kulingana na idadi ya wananchi waliopo.

UTOAJI HAKI UZIDI KUIMARISHWA HASA KWA WASIO NA UWEZO ASEMA PROF. KABUDI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko alipomtembelea ofisini kwake mjini Mpanda kabla ya kukagua mahakama za Hakimu Mfawidhi Katavi, Mahakama ya Wilaya Mpanda na Mahakama ya Wilaya Tanganyika. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiongea na watumishi wa Mkoa wa Katavi (hawapo pichani) alipotembelea ofisini hapo kabla ya kufanya ziara katika mahakama za hakimu mkazi katavi, wilaya ya mpanda na wilaya ya Tanganyika.  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na watumishi wa Mahakama alipotembelea Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi na Mahakama ya Wilaya Mpanda. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisisitiza jambo katika ziara hiyo. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akitoa ushauri wakati akikagua ujenzi wa mahakama ya Wilaya Tanganyika. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi asisi

AMANI YA NCHI NI MOJA YA MAFANIKIO KWA SEKTA YA SHERIA KATIKA MIAKA 60 YA UHURU

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akiwaelezea kuhusu sekta ya sheria ilipotoka, ilipo, inakoelekea na mafanikio iliyopata katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Prof. Kabudi.

MIAKA 60 YA UHURU

Image
 

WANANCHI WANA KIU YA KUJUA SHERIA – MASHILINDI

Image
Kaimu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe. David Mashilindi akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria baada ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria. Kaimu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe. David Mashilindi  ambaye ni mgeni rasmi akitoa hotuba kabla ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria jijini Mbeya. Kaimu Msajili wa watoa huduma ya msaada wa kisheria Wakili Ester Msambazi akitoa taarifa ya tathmini juu ya maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2021 kwa mkoa wa Mbeya kabla ya kufungwa kwa maadhimisho hayo.  Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Wakili Griffin Mwakapeje akiongea katika hafla ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria jijini Mbeya. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX “Maonyesho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria yamedhihirisha kiu ya wananchi ni kubwa kutaka kujua masuala ya sheria” Hayo yamesemwa na Kaimu Meya wa jiji la Mbeya Mhe. David Mashilindi katika hitimisho la maadhimisho ya Wiki ya Msaada

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SIDO WAKIPATA ELIMU KUHUSU UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI NA MIKOPO KUTOKA KWA MAWAKILI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MSAADA WA KISHERIA MKOANI MBEYA

Image
Wakili wa kujitegemea kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika Bi. Laetitia Ntagazwa akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la SIDO jijini Mbeya kuhusu migogoro ya ardhi na namna ya kutatua migogoro hiyo inapotokea ikiwemo kupeleka migogoro hiyo katika mabaraza ya ardhi. Elimu hii inatolewa ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya. Wafanyabiashara wa soko la SIDO jijini Mbeya wakiwasikiliza Mawakili na Wasaidizi wa Kisheria (hawapo pichani) waliofika katika soko hilo ili kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao kuhusu umiliki wa ardhi, namna ya kutatua migogoro ya ardhi na namna ya kupata mikopo kwa kuzingatia kanuni na taratibu ili kuepuka migogoro na utapeli. Wakili wa kujitegemea kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyinya Bw. Gernus Mzalila akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la SIDO juu ya umuhimu wa mikopo na namna bora ya kukopa kwa kufuata kanuni na taratibu. 

MABORESHO YA HAKI JINAI KUTATUA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI HAKI – HOMERA

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera akizungumza katika ufunguzi wa Wiki ya Msaada wa Kisheria. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera ( wa pili kushoto) akifurahia jambo wakati akipata maelezo kutoka kwa Wakili George Mollel (wa tatu kulia) alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria kabla ya kuzindua rasmi Wiki ya Msaada wa Kisheria inayofanyika kitaifa Mkoani Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera akipata maelezo alipotembelea banda la Haki za Binadamu. Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera (waliokaa katikati) baada ya uzinduzi wa Wiki ya Msaada wa Kisheria. Wananchi wakipata huduma katika mabanda mbalimbali katika viwanja vya Ruandanzovwe jijini Mbeya kwenye maonyesho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera amesema maboresho ya haki jinai yatasaidia kutatua changamoto za upatikanaji haki. Mhe. Homera ameyasema hayo wakati akizindua

WAZIRI KABUDI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE TATHMINI YA MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU GENEVA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi aongoza    ujumbe wa Tanzania kushiriki kikao cha kwanza cha tathimini ya Tanzania juu ya Masuala ya Haki za Binadamu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi tarehe 5.11.2021.

KABUDI AONGOZA KIKAO KAZI CHA NDANI OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA USWISI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiongoza kikao kazi cha ndani kilichofanyika katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, mjini Geneva, Uswisi tarehe 3/11/2021. Kikao kazi hicho kilihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania katika mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Uswisi Mhe. Maimuna Tarishi, Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu Ndg. Amon Mpanju pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na ofisi ya Balozi.