WANANCHI WANA KIU YA KUJUA SHERIA – MASHILINDI
Kaimu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe. David Mashilindi akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria baada ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria.
Kaimu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe. David Mashilindi ambaye ni mgeni rasmi akitoa hotuba kabla ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria jijini Mbeya.
Kaimu Msajili wa watoa huduma ya msaada wa kisheria Wakili Ester Msambazi akitoa taarifa ya tathmini juu ya maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2021 kwa mkoa wa Mbeya kabla ya kufungwa kwa maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Wakili Griffin Mwakapeje akiongea katika hafla ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria jijini Mbeya.
“Maonyesho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria yamedhihirisha kiu ya wananchi ni kubwa kutaka kujua masuala ya
sheria”
Hayo yamesemwa na Kaimu Meya wa jiji
la Mbeya Mhe. David Mashilindi katika hitimisho la maadhimisho ya Wiki ya
Msaada wa Kisheia katika uwanja wa RuandaNzovwe jijini Mbeya ambayo yalianza
Novemba 8 na yamefikia tamati Novemba 12 jijini mbeya.
Mhe Mashilindi amesema ana matumaini
makubwa kuwa jamii imeelimishwa kuhusu sheria mbalimbali katika maadhimisho
hayo kupitia vyombo vya habari na uwanjani ambapo elimu kuhusu mirathi, ukatili
wa kijinsia , ndoa n.k imetolewa.
Aliongeza, ana imani elimu hiyo
imefika kwa watendaji na wananchi kwa ujumla na hivyo kila mdau atimime wajibu
wake ili wananchi wapate haki kwa ubora unaostahili.
Alisema” Juhudi mbalimbali zimefanywa
kufikia wananchi lengo ni kuhakikisha
hakuna mtu anaachwa nyuma lengo likiwa ni kuboresha mfumo wa utoaji haki
jinai na kila mdau atimize wajibu wake na wananchi wapate haki kwa ubora
unaostahili”
Vilevile aliwataka wadau wote wa haki
jinai washirikiane na wasiwe vyanzo vya migogoro mahakamani na wadaiana
wanapokuwa tayari kumaliza kesi nje ya mahakama wasaidiwe.
Aidha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Katiba naSheria ambaye ni Mkujrugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma
Bw. Griffin Mwakapeje amesema Wizara ya Katiba na Sheria inaimarisha mifumo ya
kisheria na kuimarisha sera ya haki jinai.
Aliongeza marekebisho ya sharia ya mwenendo wa mashauri
ya jinai yamefanyika ikiwemo makosa ya faini kulipishwa faini ili kutimiza
lengo la Rais ambalo ni kuhakikisha mashauri ya makosa ya jinai yanamalizika
kwa haraka ili kupunguza msongamano magerezani.
Vilevile Kaimu Katibu Mkuu huyo
alitoa rai kwa wananchi wanapopata changamoto za kisheria kwenda kwa wasaidizi
wa kisheria ili kuweza kushughulikiwa matatizo yao kwa wakati na sio kukimbilia
kwa watawala.
Naye Kaimu Msajili wa Wasaidizi wa
Kisheria Bi. Ester Msambazi akitoa tathmini ya mafanikio yaliyopatikana katika
maadhimisho hayo kwa mwaka 2021 amesema elimu na msaada wa kisheria uliotolewa
maeneo ya vizuizi umewezesha mahabusu kupata dhamana na hivyo kupunguza
msongamano na kuwezesha mahabusu hao kuendelea na shughuli zao za uzalishaji
mali ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa nchi.
Comments
Post a Comment