WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SIDO WAKIPATA ELIMU KUHUSU UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI NA MIKOPO KUTOKA KWA MAWAKILI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MSAADA WA KISHERIA MKOANI MBEYA

Wakili wa kujitegemea kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika Bi. Laetitia Ntagazwa akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la SIDO jijini Mbeya kuhusu migogoro ya ardhi na namna ya kutatua migogoro hiyo inapotokea ikiwemo kupeleka migogoro hiyo katika mabaraza ya ardhi. Elimu hii inatolewa ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya.



Wafanyabiashara wa soko la SIDO jijini Mbeya wakiwasikiliza Mawakili na Wasaidizi wa Kisheria (hawapo pichani) waliofika katika soko hilo ili kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao kuhusu umiliki wa ardhi, namna ya kutatua migogoro ya ardhi na namna ya kupata mikopo kwa kuzingatia kanuni na taratibu ili kuepuka migogoro na utapeli.


Wakili wa kujitegemea kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyinya Bw. Gernus Mzalila akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la SIDO juu ya umuhimu wa mikopo na namna bora ya kukopa kwa kufuata kanuni na taratibu. 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA