Posts

Showing posts from 2022

DKT. NDUMBARO ASHIRIKI HAFLA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU WA KENYA

Image
XXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax katika Hafla ya maadhimisho ya miaka ya 58 ya Uhuru wa Taifa la Kenya yaliyofanyika tarehe 12/12/2022, Jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahaman Kinana, Amidi wa Mabalozi wa mataifa mbalimbali Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui. Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kenya, ni fursa pekee ya kuangalia mahusiano baina ya nchi hizo mbili ambapo siku zote yamezidi kuimarika kama yalivyoasisiwa na Waasisi wa Mataifa haya mawili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Jomo Kenyatta. Aidha, Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa pamoja na kwamba mahusiano katika Nyanja za Biashara yamezidi kuimarika zinahitajika jitihada zaidi na kutoa rai kwa wafanyabiashara kue...

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA MAAFISA KUTOKA UBALOZI WA UINGEREZA

Image
  XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na maafisa kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini; Dkt. Zabdiel Kimambo -Mshauri wa Utawala, Bw. Laurence Wilkes, Mshauri wa Masuala ya Utawala na Siasa, na Bi. Allanna Inserra, Mshauri wa Masuala ya Siasa tarehe 14 Desemba, 2022 katika Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho wamejadili masuala mbalimbali yahusuyo ushirikiano baina ya Serikali na Asasi za Kiraia na utekelezaji wa miradi ambayo inafadhiliwa na Uingereza kupitia Asasi mbalimbali hapa nchini. Dkt. Ndumbaro ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuwa na ushirikiano na uhusiano mzuri na Asasi za Kiraia hususan katika upatikanaji wa maoni katika sheria mbalimbali zinazohitaji kufanyiwa marekebisho.  Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Casmir Kyuki na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Griffin Mwakapeje...

DKT. DAMAS DUMBARO AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU

Image
  XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.  Damas Ndumbaro amezindua maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Bindamu kitaifa.  Maadhimisho hayo yamezinduliwa  tarehe 6 Desemba, 2022 katika viwanja vya Nyerere Square vilivyopo katikati ya mji,  jijini Dodoma.  Akiongea kwenye  Uzinduzi   huo Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema "Maadhimisho haya yameanza mwaka 2016  kwa lengo la kuwa na siku ya kimataifa ya kupambana na Rushwa pamoja na siku ya kimataifa ya Haki za Binadamu  ili kuwaelimisha wananchi namna ya kupiga vita rushwa  na  pia  juu ya masuala ya Haki za Binadamu." Pia Dkt. Ndumbaro amesema "Jukumu kubwa la Serikali yetu ni kuwaletea Wananchi  maendeleo, hivyo Usimamizi wa Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Uwazi na mapambano dhidi ya rushwa  ni masuala endelevu kwa kuwa ni msingi wa utoaji huduma bora kwa Umma." Kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema _"Maadili, Haki za Binadamu, Utawala Bo...

HATUA KALI ZAIDI KUCHUKULIWA KWA WAHALIFU WA MAKOSA YA UNYANYASAJI KIJINSIA: DKT. NDUMBARO

Image
XXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali imejipanga kuchukua hatua kali zaidi kwa wahalifu wa makosa ya unyanyasaji kijinsia. Waziri Ndumbaro ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) Novemba 5, 2022 Jijini Dar es Salaam. Dkt. Ndumaro amesema “rai ya Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kupaza sauti siku zote 365 za mwaka kutambua viashiria vya unyanyasaji wa kijinsia na kuvitolea taarifa kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake.” Katika hatua nyingine Mhe. Ndumbaro amesema “Wizara ya Katiba na Sheria iko mbioni kuanzisha usajili wa mtandaoni (online registry) kwa mtu ambaye amethibitishwa na Mahakama kuwa na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia.” Watu watakaokuwa katika orodha hiyo hawatakuwa na uwezo wa kukopa benki wala kupata ajira, miongoni mwa huduma zingine. Kwenye maadh...

WAZIRI NDUMBARO ASHIRIKI HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA KITUO JUMUISHI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza, Novemba 29, 2022.  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Khatibu Kazungu akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza, Novemba 29, 2022.  XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza leo Novemba 29, 2022.  Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu, Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Patience Ntwina. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro amepongeza jitihada hizo na ushirikiano u...

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KUANDAA MPANGO KAZI WA UFUATILIAJI NA TATHIMINI.

Image
 XXXXXXXXXXX Wizara ya Katiba na Sheria inaandaa Mpango Kazi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa mwaka wa shughuli zote za Wizara.  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera, Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini ndugu Emmanuel Mayeji kwenye kikao kazi cha siku tano kinachofanyika kuanzia tarehe 28 Novemba hadi 2 Desemba 2022 mjini Morogoro.  Ndugu Mayeji  amesema " kakao hiki  kina malengo makuu mawili , Moja  kujadili namna ya kuwa na mfumo thabiti wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni , Miongozo na Mipango inayosimamiwa" Mbili kuwa na mfumo  thabiti wa utoaji wa taarifa  za utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kuzingatia takwimu sahihi za mafanikio na changamoto zilizojitokeza pamoja na kuwa na  mkakati wa kutatua changamoto zilizojitikeza wakati wa utekelezaji" . Aidha kikao kazi hicho kinahudhuriwa na  maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

JIUNGENI NA CHAMA CHA MAWAKILI CHA AFRIKA MASHARIKI- MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Image
  XXXXXXXXXXXXX Rais Samia Suluhu Hassan  amewataka Mawakili  nchini kujiunga na Chama Cha Mawakili Cha Afrika Mashariki (East Africa Law Society). Mheshimiwa Rais ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa  Chama Cha Mawakili Cha Afrika Mashariki tarehe 24 Novemba, 2022 Jijini Arusha . Akiongea kwenye kikao hicho Mhe. Rais amesema "Afrika Mashariki Sasa ni wamoja tunafanya kazi kwa kushirikiana, na nyinyi shirikianeni kutatua kesi mbalimbali ndani ya Jumuiya yetu na nje ya Jumuiya, kuweni wamoja na imara  katika kujenga Chama chenu"  Aidha Mheshimiwa Rais amewaomba Mawakili  kuwakaribisha Mawakili kutoka DRC Congo , ambao wamejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki hivi karibuni.  Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda  ambaye alimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  amesema " ni fursa kwa Mawakili   wetu kufanya kazi ndani ya Afrika Mashariki kwasababu watajijeng...

KIKAO KAZI

Image
  XXXXXXXXXXXXX Wataalam kutoka Wizara ya Katiba na sheria na Taasisi zilizo chini yake wakutana mjini Morogoro kwa kikao kazi cha siku tano kuanzia Novemba 22 hadi 26, 2022 kuandaa vipaumbele vya Wizara kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024. Pia katika kikao hicho watajadiliana  kuhusu maandalizi ya kuanza Kwa awamu ya pili ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Mtaalam Mwelekezi alipofanya utafiti juu ya changamoto zinazoikabili sekta ya sheria.

DKT. NDUMBARO ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

Image
 XXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro anashiriki Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Mjini Balaclava, nchini Mauritius kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba, 2022. Mkutano huo umefunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Pravind Kumar Jugnauth. Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali katika sekta ya sheria yakiwemo masuala ya upatikanaji haki, Haki za Binadamu, matumizi ya akili bandia katika mifumo ya Mahakama, umuhimu wa sekta ya sheria katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Mambo mengine yanayotarajiwa kujadiliwa katika Mkutano huo ni Urejeshwaji wa Wahalifu, Mikataba ya Uwekezaji, Hatua zilizochokuliwa na Nchi Wanachama katika maeneo mbalimbali yakiwemo Mapambano dhidi ya Rushwa, Sheria za Kudhibiti uhalifu wa mtandao, Ushirikiano katika masuala ya Jinai na Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala na  wajibu wa Vyombo vya Habari katika kutekeleza Haki ya Kutoa Maoni...

MALALAMIKO YA WANAFUNZI WA LAW SCHOOL HAYANA USHAHIDI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akipokea ripoti ya tathmini ya mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (law school) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Makondo. Dkt. Ndumbaro akikabidhi ripoti kwa Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo. Dkt. Ndumbaro akikabidhi ripoti kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu. Mwenyekiti wa Kamati Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia) akielezea jambo. Picha ya Viongozi wa wizara na Wajumbe wa Kamati. XXXXXXXXXXXXXXXX Kamati ya Tathmini ya Mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Kwa Vitendo Tanzania yakosa ushahidi wa kuthibitisha tuhuma za rushwa, uonevu na upendeleo katika utungaji na usahihishaji wa mitihani zilizotolewa na wanafunzi wa kundi la 33. Hayo yamebainishwa Leo Novemba 20, 2022 wakati Kamati hiyo ikikabidhi ripoti ya tathmini hiyo Kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbar...

JUKUMU LA KUHIFADHI WAKIMBIZI SIYO JEPESI HASA KWA NCHI WENYEJI- MHE PINDA

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey  Pinda   akifunga kikao kazi cha siku tatu cha kujadili masuala mbalimbali ya Wakimbizi na Wahamiaji kilichofanyika jijini, Arusha. Washiriki wa kikao. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXXXXXX Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey  Pinda amesema  kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na  changamoto  ya kuwa na idadi kubwa ya watu wanaokimbia makazi yao  jukumu la kuhifadhi Wakimbizi ni jukumu zito hasa kwa nchi inayopokea Wakimbizi.  Mhe. Pinda ameyasema hayo  wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha kujadili masuala mbalimbali ya Wakimbizi na Wahamiaji kilichofanyika  kuanzia tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 jijini Arusha. Katika kikao hicho Mhe. Pinda amesema " Serikali imekuwa ikihifadhi Wakimbizi kwa muda mrefu, hivyo inatambua mchango mkubwa wa wadau wa masuala ya Wakimbizi katika nyanja zote". Aidha, Mhe. Pinda amesema "kama mnavyofahamu  Wakimbizi wengi...

DKT. NDUMBARO AIASA JAMII KUACHA VITENDO VYA UKATILI

Image
Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya akifungua kikao cha mtandao wa masuala ya familia kuhusu upatikanaji wa sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia. Meza kuu. Washiriki. Picha ya pamoja.  XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameiasa jamii kuachana na Vitendo vya ukatili wa kijinsia. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya kwa niaba ya Dkt. Ndumbaro katika ufunguzi wa kikao cha mtandao wa masuala ya familia na Wadau kutoka  Wizara  mbalimbali kuhusu upatikanaji wa sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika Novemba 16, 2022 mjini Morogoro. Amesema, "kama tunataka kuwa na jamii imara, ni lazima sote tuungane na kupinga Vitendo vyovyote vya ukatili" Vilevile, katika hotuba yake Dkt. Ndumbaro amewataka Wadau hao kusaidiana na serikali kutoa elimu na kuendelea kukemea vitendo vya ukatili kwani h...

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA IMEJIPANGA KUBORESHA MIUNDOMBIMU YA MAHAKAMA

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya ya Mwanga na Same.     XXXXXXXXXXXXXXXX Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey Mizengo Pinda amesema  Wizara imejipanga kuhakikisha miundombinu ya Mahakama inakuwa bora. Mhe. Pinda amesema hayo jana tarehe 15 Novemba, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya ya Mwanga na Same. Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Pinda amesema "Serikali  yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan   inahakikisha mazingira ya utoaji haki katika Mahakama zetu yanakuwa bora na rafiki, na tayari kwa mwaka huu tunashuhudia Mahakama mbalimbali zikijemgwa,  tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais." Aidha, Jaji Mkuu Mheshimiwa Prof. Ibrahimu Juma amesema Mahakama imejiwekea mkakati kuhakikisha  inaendelea kujenga majengo ya Mahakama kwa zile Wilaya ambazo majengo yao yamechakaa ili kuhakikisha...

TAASISI ZA HAKI JINAI ZAANDAA MFUMO WA KUBADILISHANA TAARIFA

Image
Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Ernest Mbuna akitoa mada katika kikao cha maandalizi ya mfumo wa Haki Jinai. Washiriki wa kikao kazi. Washiriki wa kikao kazi. XXXXXXXXXXXXXX Wataalam wa Sheria na TEHAMA kutoka Taasisi za Haki Jinai wamekutana mjini Morogoro ili kuandaa mahitaji ya mfumo wa kabadilishana taarifa miongoni mwa Taasisi hizo nchini. Kikao hicho  kimeandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kikiwa na lengo la kuwezesha taasisi za Haki jinai kuwa na mifumo thabiti inayosomana na kufanikisha maamuzi yanayofanyika kwenye mfumo wa Haki jinai kuwa yenye tija. Aidha, kikao hicho kitawezesha kujua mifumo iliyopo katika Taasisi ya kuwezesha kubadilishana taarifa, kujua taarifa ambazo zinahitajika kubadilishana baina ya Taasisi na kukubaliana maeneo ya kuhifadhi mifumo itakayowezesha kubadilishana taarifa. Taasisi zinazoshiriki kwenye kikao hicho ni Mahakama, Polisi, Magereza, Mkemia Mkuu,  Wizara ya mambo ya Ndani, Uhamiaji, Ustawi wa Jamii, TAKUKURU, ...

WANANCHI KUNUFAIKA NA UTAJIRI ASILI NA MALIASILIA ZA NCHI- MHE. PINDA

Image
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akifungua kikao kazi cha kuandaa mkakati jumuishi wa utekelezaji wa Sheria za Mamlaka ya Nchi kuhusu Umiliki wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 449 na Sheria ya Mapatano na Majadiliano kuhusu masharti hasi   katika Mikataba ya Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 450. Mkurugenzi wa Kitengo Cha Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia za Nchi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Bi. Neema Mwanga  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akufungua kikao kazi   Washiriki wa kikao kazi. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXX Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amewataka washiriki wa kikao kazi Cha kuandaa mkakati jumuishi wa utekelezaji wa Sheria za Mamlaka ya Nchi kuhusu Umiliki wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 449 na Sheria ya Mapatano na Majadiliano kuhusu masharti hasi   katika Mikataba ya Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 450, kuandaa m...

WAZIRI NDUMBARO AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA WIZARA JIJINI DODOMA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akitoa maelekezo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma.   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha wataalam wa ujenzi na menejimenti ya wizara ili kupata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha wataalam wa ujenzi na menejimenti ya wizara ili kupata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria linaloendelea kujengwa Mtumba, jijini Dodoma. Dkt. Ndumbaro amefanya ukaguzi huo Leo Novemba 04, 2022 baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kamati ya ujenzi ya Wizara na Kwa Mkand...

WATUMISHI KATIBA NA SHERIA WATAKIWA KUCHAPA KAZI NA KUZINGATIA UADILIFU NA NIDHAMU

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na watumishi wa Wizara hiyo. Viongozi waliowahi kuongoza katika wizara hiyo kwa nafasi mbalimbali wakikabidhiwa zawadi. Watumishi wastaafu wakikabidhiwa zawadi. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kuelewa majukumu waliyonayo si lelemama hivyo wayatekeleze kwa kuzingatia uchapakazi, uadilifu, nidhamu na kufanya kazi kama timu ili kuweza kuleta matokeo mazuri ya kazi zao. Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Novemba 3, 2022 jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na watumishi hao kabla ya hafla ya kuwaaga viongozi na watumishi wa Wizara hiyo waliostaafu. Waziri Ndumbaro amesema ‘’Wizara hii ni wizara kubwa na nyeti kwa sababu imeshikilia Katiba ya nchi, pia inashughulika na sheria ambayo ndiyo kila kitu katika utawala wa nchi’’ Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa ‘’Nataka muelewe kwamba jukumu tulilonalo si lelemama tutaweza kulitekeleza tukizingatia uchapaka...