Posts

Showing posts from January, 2022

WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA BODI YA KITAIFA YA USHAURI WA MSAADA WA KISHERIA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (wa nne kushoto) akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Makondo (wa nne kulia) na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu (wa pili kushoto) afanya majadiliano na Bodi ya Kitaifa ya Ushauri wa Msaada wa Kisheria ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo Bw. Saulo Malauri na Katibu wa Bodi  ambaye pia ni msajili wa Watoa Msaada wa Kisheria Bi. Felistas Mushi. Majadiliano hayo yamefanyika leo Januari 28, 2022.

JAJI MKUU NA JAJI KIONGOZI WA TANZANIA WATEMBELEA BANDA LA WIZARA KWENYE MAONYESHO YA WIKI YA SHERIA

Image
 Jaji  Mkuu wa Mahakama Mhe. Prof. Ibrahim Juma akipata maelezo kutoka kwa Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Anne Malipula kutoka Wizara ya Katiba na Sheria alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. Jaji kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Mustapha Siyani akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria kwenye maonyesho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

MKUTANO WA KAMATI YA MAWAZIRI WA SHERIA WA SADC WAFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

Image
  Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akiwa katika picha ya pamoja na wataalam baada ya mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria/Wanasheria Wakuu wa nchi zilizoko kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

VIONGOZI WA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA WAMTEMBELEA WAZIRI SIMBACHAWENE OFISINI KWAKE

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Bw. Sylvester Mwakitalu (wa pili kushoto) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Gabriel Malata (wa pili kushoto) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  walioambatana na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo waliofika ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma. 

VYOMBO VYA UPELELEZI MSIHARIBU MALI MNAZOKAMATAKABLA YA KESI KUMALIZIKA - MHE. GEOPHREY PINDA

Image
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho katika Wiki ya Sheria inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. Naibu   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey  Pinda akipata maelezo katika banda la Mahakama alipotembelea mabanda ya maonyesho  katika Wiki ya Sheria.  Naibu  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la kitengo cha maboresho katika mahakama ya Tanzania. Naibu  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akimsikiliza mwananchi aliyefika katika maonyesho ya Wiki ya Sheria katika kitengo cha malalamiko cha Mahakama ya Tanzania. Naibu  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara hiyo wanatoa huduma katika banda la wizara kwenye maonyesho ya Wiki ya Sheria.

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI AZINDUA WIKI YA SHERIA JIJINI DODOMA

Image
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Wakili wa Serikali Dkt. Anne Malipula alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akizindua bendera ya Mahakama katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiongoza maandamano yaliyoshirikisha viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene kabla ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiongoza waandamanaji kufanya mazoezi ya viungo kabla ya kuanza maandamano kuelekea viwanja vya Nyerere Square kwenye uzinduzi wa Wiki ya Sheria. Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika banda la Wizar...

WAZIRI SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akiongoza kikao cha manejimenti ya wizara na kupata taarifa ya utekelezaji. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Kazungu Khatibu (aliyesimama) akiongea katika kikao cha menejimenti ya wizara hiyo kilichoongozwa na Waziri Simbachawene. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (kushoto) akifuatilia taarifa za utekelezaji wa majukumu ya wizara zinazotolewa wakuu wa idara na vitengo wa wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha menejimenti ya wizara hiyo. Mwingine pichani ni Naibu Waziri Mhe. Geophrey Pinda   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa za utekelezaji wa majukumu zinazotolewa na wajumbe wa menejimenti katika kikao cha menejimenti ya wizara hiyo.

KATIBU MKUU BI MARY MAKONDO AKAGUA UJENZI WA OFISI ZA WIZARA YA KATIBA

Image
 Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa ujenzi alipotembelea eneo la ujenzi  wa ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria ili kujionea hali ilivyo na hatua iliyofikiwa. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akikagua vifaa vya ujenzi vinavyotumika kwenye ujenzi wa ofisi za Wizara hiyo unaoendelea Mtumba, jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akiwa ameongozana na viongozi  akiwemo Naibu Katibu Mkuu Dkt  Kazungu Khatibu na menejimenti ya wizara hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za wizara zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.

WAZIRI, KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU WAPOKELEWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Image
Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto), Naibu Waziri wa Katibu na Sheria Mhe. Geophrey Pinda (wa pili kushoto), aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (mwenye tai ya njano) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Issa Ng'imba wakibadilishana mawazo wakati wakisubiri kuwapokea viongozi wapya walioteuliwa kuiongoza wizara hiyo ili kukabidhiana ofisi. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba, jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba, jijini Dodoma. Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiandaa nyaraka mbalimbali kwa ajili ya makabidhiano ya ofisi na Katibu Mkuu mpya (hayupo pichani) aliyeteuliwa kuiongoza Wizara hiyo. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. G...