RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI AZINDUA WIKI YA SHERIA JIJINI DODOMA


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Wakili wa Serikali Dkt. Anne Malipula alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akizindua bendera ya Mahakama katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiongoza maandamano yaliyoshirikisha viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene kabla ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiongoza waandamanaji kufanya mazoezi ya viungo kabla ya kuanza maandamano kuelekea viwanja vya Nyerere Square kwenye uzinduzi wa Wiki ya Sheria.
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika banda la Wizara hiyo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria.

Mawakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi Anne Malipula ( kushoto) na Bi Ester Msambazi wakiwa katika banda la wizara hiyo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria.

Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA