WAZIRI, KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU WAPOKELEWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto), Naibu Waziri wa Katibu na Sheria Mhe. Geophrey Pinda (wa pili kushoto), aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (mwenye tai ya njano) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Issa Ng'imba wakibadilishana mawazo wakati wakisubiri kuwapokea viongozi wapya walioteuliwa kuiongoza wizara hiyo ili kukabidhiana ofisi.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.


Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiandaa nyaraka mbalimbali kwa ajili ya makabidhiano ya ofisi na Katibu Mkuu mpya (hayupo pichani) aliyeteuliwa kuiongoza Wizara hiyo.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akiwa ameshikilia maua aliyokabidhiwa na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria ikiwa ni ishara ya ukaribisho katika kuitumikia wizara hiyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akipokea maua kutoka kwa Katibu Mahsusi Bi. Dina Njovu  wakati watumishi wa Wizara hiyo walipomkaribisha wizarani hapo kwa mara ya kwanza  baada ya kuteuliwa, anayeshuhudia pembeni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Makondo.

 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA