Posts

Showing posts from March, 2022

"HUKUMU ZINAZOTOLEWA MAHAKAMANI ZITEKELEZWE KWA WAKATI" WAZIRI SIMBACHAWENE

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akizindua ripoti ya wadau ya upatikanaji haki baada ya kufungua Kongamano la Msaada wa Kisheria la mwaka 2022. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa kitengo cha  Msaada wa Kisheria ambaye pia ni Msajili wa Watoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Felistas Mushi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Huduma za Kisheria Bi. Lulu Ng'w'anakilala. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akipata maelezo kutoka kwa Wakili Neema Ahmed ambaye ni Mratibu wa TAWLA Mkoani Dodoma kabla Waziri Simbachawene hajafungua Kongamano la Msaada wa Kisheria linalofanyika jijini Dodoma. Wakili wa Serikali Bi. Lilian Kilembe akitoa huduma kwa mteja Bw. Benjamin Sembelu aliyefika kwenye banda la Wizara hiyo ili kupata msaada wa Kisheria wakati wa Kongamano la Msaada wa Kisheria jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene ataka kesi zilizotolewa maamuzi na mahakama maamu

MHE. GEOPHREY PINDA AONGOZA KIKAO KATI YA WIZARA NA TAASISI

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akiongoza kikao kati ya Wizara na Taasisi zake wakijadili kuhusu utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa mwaka 2021/2022 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2022/2023. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akizungumza katika kikao kati ya Wizara na Taasisi zake wakijadili kuhusu utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa mwaka 2021/2022 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2022/2023. Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bi. Elizabeth Tagora akifafanua jambo  katika kikao kati ya Wizara na Taasisi zake wakijadili kuhusu utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa mwaka 2021/2022 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2022/2023. Sehemu ya Washiriki wa kikao hicho.

TANZANIA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE KATIKA KUTEKELEZA HAKI ZA BINADAMU UN

Image
 

PONGEZI

Image
 

KAMATI YA KITAIFA YA MAUAJI YA KIMBARI

Image
 

KUMBUKIZI

Image
 

WAZIRI SIMBACHAWENE AELEZEA MAFANIKIO 11 YA MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA SEKTA YA SHERIA

Image
Waziri wa katiba na sheria Mhe.George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akieleza mafanikio ya Wizara yake ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita.   Waziri wa katiba na sheria Mhe.George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari wakati akieleza mafanikio ya Wizara yake ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita . Baadhi ya waandishi wa habari waloihudhuria kikao. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa katiba na sheria Mhe.George Simbachawene ametaja maeneo ambayo Wizara yake inajivunia kufanya vizuri kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani. Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2022 katika mkutano maalum, Waziri Simbachawene amesema Wizara yake imefanya mambo mengi katika kuwatumikia Watanzania ambapo katika hayo ina maeneo yaliyofanikiwa zaidi. “ Kwa upande wangu kama Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria, nitazungumzia mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Sheria kwa kipindi cha mwaka

MAPUNGUFU YA KIUTENDAJI YABAINISHWE ILI KUBORESHA UTENDAJI KAZI - SIMBACHAWENE

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akifungua baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo jijini Dar Es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheriaambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo Bi. Mary Makondo akiongea baada ya ufunguzi wa baraza hilo. Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea na kikao cha baraza. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kulifungua. XXXXXXXXXXXXXXXXXXX Baraza la wafanyakazi wa wizara ya katiba na sheria limetakiwa kuwa wazi,kutoa mapendekezo, na kukosoa mahala ambapo kuna Mapungufu ya kiutendaji ili kuweza kuboresha wizara hiyo katika utendaji wa kazi. Akizungumza leo Alhamisi Machi 10,2022 Wakati akifungua mkutano wa baraza hilo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geogre Simbachawene amesema kuwa ni vema wafanyakazi wakawa wazi Kuzungumza kama kuna mapungufu mahali ili w

MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WAKUTANA NA WAZIRI SIMBACHAWENE

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akizungunza katika kikao na baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu walipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu walipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

TANGAZO

Image
 

WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA WASAIDIZI WA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA

Image
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akutana na kuzungumza na Wasaidizi wa Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara wakati wa kikao chao cha siku mbili jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.

TANZANIA INATAMBUA WAJIBU WA KUKUZA NA KULINDA HAKI ZA BINADAMU - SIMBACHAWENE

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma kuhusu Kikao cha 49 cha Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu kilichofunguliwa Februari 28, mwaka huu na yeye alihutubia Baraza hilo Machi 2, mwaka huu kwa njia ya video. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa Tanzania  inatambua wajibu wake mkuu wa kulinda na kukuza haki za binadamu kama mwanachama wa Umoja wa Taifa (UN) na Baraza la Haki za Binadamu. Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kikao cha 49 cha Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu alikichofunguliwa Februari 28, mwaka huu na yeye alihutubia Baraza hilo Machi 2, mwaka huu kwa njia ya video. Simbachawene amesema kuwa Serikali ipo imara na inafanya jitihada za makusudi kuhakikisha haki za msingi na uhuru wa kidemokrasia, haki za kiraia na za kisiasa zinaheshimiwa na pia kuna mazingira wezeshi ya kukuza ha