MAPUNGUFU YA KIUTENDAJI YABAINISHWE ILI KUBORESHA UTENDAJI KAZI - SIMBACHAWENE


 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene akifungua baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo jijini Dar Es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheriaambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo Bi. Mary Makondo akiongea baada ya ufunguzi wa baraza hilo.



Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea na kikao cha baraza.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kulifungua.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Baraza la wafanyakazi wa wizara ya katiba na sheria limetakiwa kuwa wazi,kutoa mapendekezo, na kukosoa mahala ambapo kuna Mapungufu ya kiutendaji ili kuweza kuboresha wizara hiyo katika utendaji wa kazi.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 10,2022 Wakati akifungua mkutano wa baraza hilo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geogre Simbachawene amesema kuwa ni vema wafanyakazi wakawa wazi Kuzungumza kama kuna mapungufu mahali ili wizara iweze kuboresha zaidi.

“Mnaposikia jambo lolote lazima mlifanyie kazi, mkisifiwa mjue kazi mnayoifanya iko vizuri lakini mkisikia mmesemwa vibaya mjitafakari mjue wapi mnakosea ili muweze kujirekebisha na mambo mengine yaende”. Amesema 

Aidha Waziri Simbachawene amewataka wafanyakazi hao kutimiza majukumu yao ya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha wizara hiyo inasonga mbele kwa kuwa na umoja wa kazi katika kuwaletea maslahi watanzania.

Katika hatua nyingine Simbachawene amesema kuwa ni vema kubadilisha mfumo wa upimaji wa watumishi wa umma kwa kufanya utafiti ili kuongeza ufanisi wa kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni katibu mkuu wa wa Wizara hiyo Mhe. Mary Makondo ameahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Waziri na kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili kuweza kutimiza malengo yaliyopo kwenye bajeti ya Wizara hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA