Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akiongea na Wahariri na Waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya namna ya utoaji wa taarifa za ukatili wa kijinsia , leo 17 Mei, 2022. katika ukumbi wa Mt. Meru Arusha. Mkurugenzi wa Idara ya Utoaji Huduma za Kisheria Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Griffin Mwakapeje akitoa salamu za ukaribisho kwa mgeni Rasmi na Wahariri na Waandishi wa Habari wanaohudhuria mafunzo ya namna ya utoaji taarifa za ukatili wa kijinsia, leo 17 Mei, 2022 katika ukumbi wa Mt. Meru Arusha. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo amefungua mafunzo ya siku mbili ya namna ya utoaji taarifa za ukatili wa kijinsia kwa Wahariri na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini. Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 17 Mei, 2022 Jijini Arusha. Akifungua mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Makondo amesema lengo la mafunzo ni kujengeana uwezo, kujifunza, kubadilishana uzo...