KM KATIBA NA SHERIA AZINDUA BARAZA JIPYA LA WAFANYAKAZI IJA


                                             xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Uzinduzi huo umefanyika Mei 5, 2022.

Bi. Makondo ametoa pongezi kwa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kuwa miongoni mwa taasisi chache zinazoongoza nchini kuendesha mafunzo kwa njia ya Mtandao. 

Bi. Makondo ameahidi kuwa Wizara anayoiongoza iko tayari kutoa ushirikiano unaostahili kwa Chuo wakati wowote watakapouhitaji.

Aidha, àlitumia hafla hiyo kutoa wito kwa waajiri wote wanaoajiri wanasheria katika utumishi wa umma kuwapeleka watumishi hao kupata mafunzo katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa mujibu wa matakwa ya Waraka wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Waraka Namba 5 wa mwaka 2012. 

Hafla hiyo ya uzinduzi ilikamilika kwa wajumbe kupewa mafunzo ya siku moja ya Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma pamoja na Maadili ya Utumishi wa Umma mafunzo ambayo yameendeshwa na wawezeshaji wabobezi kutoka Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi ya Umma.

Lengo la mafunzo hayo ni kuleta tija kwa watumishi, taasisi na taifa ili kuweza kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza katika utumishi wa mma kwa kuwa Baraza la wafanyakazi ni kioo na mwanga wa taasisi

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA