TUNATAKA KUONA MALENGO YA MFUMO WA UANGALIZI WA UTAJIRI WA ASILI NA MALIASILIA ZA NCHI YANAFIKIWA: KATIBU MKUU WA WIZARA YA KATIBA NA SHERI




Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akifunga kikao kazi cha wataalam cha kufanya mapitio ya  mfumo wa Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia za Nchi.

Picha ya pamoja.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo ,ameitaka sekretariati inayosimamia utengenezaji wa mfumo wa Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia za Nchi inafanya kazi hiyo ipasavyo ili mfumo huo ukamilike kwa wakati na malengo yake yafikiwe, Bi. Makondo ametoa agizo hilo  Mei 25, 2022 mkoani Morogoro wakati akifunga Kikao kazi cha Wataalam cha kufanya mapitio ya Mfumo huo.
Mfumo huo una lengo la kusaidia utambuzi wa maliasilia za nchi na kusajili Mikataba inayoingiwa kati ya Serikali  na Wawekezaji kwenye eneo la maliasilia za Nchi. Akitaja faida zitokanazo na matumizi ya mifumo, Katibu Mkuu alitaja faida hizo kuwa ni pamoja na kuleta maboresho katika kutoa huduma na kutoa huduma kwa haraka.

Aidha, Bi. Makondo amesisitiza kuhusu Serikali ilivyojikita katika kusimamia utunzaji wa maliasilia za Nchi kutokana na faida zake kwenye uwekezaji lakini pia katika kutoa malighafi za kuzalishia bidhaa mbalimbali. Kutokana na umuhimu huo amefananisha maliasilia kama injini ya maendeleo.

Bi. Makondo amezitaka Sekta zinazosimamia utajiri asili na maliasilia za nchi kushirikiana na Wizara katika kusimamia utajiri huu wa asili kwa faida ya nchi na vizazi vijavyo. 

Kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na Wataalam katika kuboresha mfumo ameagiza Sekretarieti inayosimamia usanifu wa mfumo kuyafanyia kazi mapendekezo hayo mapema ili kuwezesha mfumo kukamilika. Amesisitiza suala la integration ya mfumo na mifumo mingine pindi utakapoanza kutumika ili kuoanisha ubadilishanaji wa taarifa.

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu, Mkurugenzi Kitengo cha Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia za Nchi SACP. Neema M. Mwanga amewapongeza watengenezaji wa mfumo kwa kazi kubwa waliyofanya. “Pamoja na ugumu wa kuanzisha kitu kipya lakini sasa mfumo umefikia hatua ya kuweza kupokea taarifa,” Bi. Mwanga

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA