WAZIRI NDUMBARO AHIMIZA MASHIRIKIANO NA UMOJA WA MATAIFA KATIKA MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake mtumba, jijini Dodoma. Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic akiongea na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani). Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amehimiza ushirikiano na Umoja wa Mataifa katika masuala yanayohusu haki za binadamu. Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo katika kikao na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic aliyetembelea ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, Dodoma leo Juni 28, 2022. "Serikali ni mtetezi namba moja wa haki za binadamu na ipo tayari wakati wowote kutoa ufafanuzi na kujibu hoja zinazohusu haki za binadamu, ili kuwatoa wasiwasi wadau wetu ikiwemo Umoja wa Mataifa na kuendeleza mashirikiano mema" alisema Dkt. Ndumbaro Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Ma...