Posts

Showing posts from June, 2022

WAZIRI NDUMBARO AHIMIZA MASHIRIKIANO NA UMOJA WA MATAIFA KATIKA MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU

Image
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na    Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake mtumba, jijini Dodoma.       Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic akiongea na  Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro  (hayupo pichani). Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amehimiza ushirikiano na Umoja wa Mataifa katika masuala yanayohusu haki za binadamu. Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo katika kikao na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic aliyetembelea ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, Dodoma leo Juni 28, 2022. "Serikali ni mtetezi namba moja wa haki za binadamu na ipo tayari wakati wowote kutoa ufafanuzi na kujibu hoja zinazohusu haki za binadamu, ili kuwatoa wasiwasi wadau wetu ikiwemo Umoja wa Mataifa na kuendeleza mashirikiano mema" alisema Dkt. Ndumbaro Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milis

KIKAO CHA TATHMINI YA YA MPANGO WA USAJILI WA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO MKOANI MANYARA

Image
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo (katikati), Kabidhi Wasii Mkuu RITA Bi. Angela Anatory (kulia), washiriki kikao cha tathmini ya mpango wa Usajili wa Watoto wa chini ya umri wa miaka mitano mkoani Manyara. Pichani yupo pia Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Makongoro Nyerere (wa pili kulia).

VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA WAWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO TLS.

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro(Mb) amewahakikishia Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ushirikiano kutoka Serikalini kupitia Wizara ya Katiba na Sheria.   Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo leo tarehe 24 Juni, 2022 Jijini Dodoma, wakati wa mazungumzo na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria wa Tanganyika wakiongozwa na Rais wa chama hicho, Prof. Edward Hosea.   Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geofrey pinda amewapongeza viongozi wa TLS kwa kuaminiwa na kuwataka wawatumikie wanachama kwa juhudi na ubunifu ili kuleta mabadiliko chanya.   Naye Katibu Mkuu, Bi. Mary Mkondo amesema milango ya Wizara ipo wazi muda wote kwa jambo lolote litakalo hitaji ushirikiano ili kuleta maendeleo kwa wananchi na kuzingatia Haki.   Rais wa TLS, Prof. Edward Hosea ameishukuru Serikali kwa utayari wake wa kushirikiana TLS katika mambo mbalimbali yaliyo ainishwa kweye kikao hicho, ikiwa ni pamoja na kutoa h

TANGAZO KWA UMMA

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA   Telegramu: "LEGAL" Simu Na.: +255 26 2310019 Nukushi: +255 26 2310056 Barua Pepe: km@sheria.go.tz DodomaTovuti: www.sheria.qotz   TANGAZO KWA UMMA   Kwa mujibu wa Kanuni ya 14(1), (2) na (3) ya Kanuni za Ithibati ya Waendesha Maridhiano, Majadiliano, Upatanishi na Usuluhishi, 2021 (Reconciliation, Negotiation, Mediation and Arbitration (Practitioners Accreditation), 2021 imetoa mamlaka kwa Msajili wa waendesha Maridhiano, Majadiliano, Upatanishi na Usuluhishi kutoa taarifa kwa watu waliowasilisha maombi ya kusajiliwa kuwa waendesha Maridhiano, Majadiliano, Upatanishi na Usuluhishi na Taasisi zinazojihusisha na utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kuhusu uamuzi uliofanywa na Jopo la Ithibati kuhusiana na maombi husika. Kwa msingi huo, Msajili wa watoa huduma za Maridhiano, Majadil