WAZIRI NDUMBARO AAGIZA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA MAHAKAMA YA HYDOM KABLA YA JUNI 19, 2022.


 
Waziri Dkt. Ndumbaro atembelea mahakama ya Hydom wilayani Mbulu.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXX


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameagiza kukamilika haraka kwa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo inayojengwa kwenye eneo la Hydom wilayani Mbulu na kuanza kutoa huduma ifikapo June 30, 2022 ili kuokoa wananchi wanaofuata huduma za kimahakama umbali wa hadi kilomita 86 na kutumia zaidi ya Shilingi laki moja kwa mwezi.

Dkt. Ndumbaro ametoa agizo hilo tarehe 5 Juni, 2022 wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM Hydom wakitaka kujua lini Mahakama hiyo itaanza kazi.

" Mheshimiwa Hakimu upo hapa na Mkurugenzi natoa maelekezo hakikisheni ifikapo June 19, 2022 ujenzi uwe umekamilika na June 30, 2022 Mahakama ianze kutoa huduma kwa wananchi, isipokamilika nitakuja mwenyewe kujua nani huyo anayekwamisha mchakato wa Mahakama hii kukamilika na kutoa huduma kwa wananchi wa Hydom" alisema Dkt. Ndumbaro.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amewataka Wananchi kuitumia Mahakama hii kuleta amani na kutenda haki kwa wananchi.

Naye Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini, Mhe. Flatey Maasay ameeleza kuwa wananchi wa eneo la Hydom hulazimika kutembea umbali wa hadi kilomita 86 kufuata huduma hizo za kimahakama eneo la Mbulu mjini na wakati mwingine kushindwa kurudi hivyo kulazimika kulala na kutumia gharama zaidi

" hapa sisi kama wananchi husafiri kilomita 86 hadi Mbulu mjini kwenda na kurudi ni Shilingi elfu 12 na wakati mwingine shughuli za kimahakama huchelewa kuisha na kupelekea mtu kulala Mbulu kwani magari ya kurudi Hydom huishia kati ya saa tisa na saa kumi jioni" alisema Mhe. Maasay

Nao wananchi wa eneo la Hydom wamepongeza na kushukuru Serikali kwa kujenga Mahakama hiyo kwani wamekuwa wanapata tabu sana kusafiri umbali mrefu. 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA