WAZIRI NDUMBARO AHIMIZA MASHIRIKIANO NA UMOJA WA MATAIFA KATIKA MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake mtumba, jijini Dodoma.
 




  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic akiongea na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani).



Picha ya pamoja.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amehimiza ushirikiano na Umoja wa Mataifa katika masuala yanayohusu haki za binadamu.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo katika kikao na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic aliyetembelea ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, Dodoma leo Juni 28, 2022.

"Serikali ni mtetezi namba moja wa haki za binadamu na ipo tayari wakati wowote kutoa ufafanuzi na kujibu hoja zinazohusu haki za binadamu, ili kuwatoa wasiwasi wadau wetu ikiwemo Umoja wa Mataifa na kuendeleza mashirikiano mema" alisema Dkt. Ndumbaro

Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ndugu Zaltan Milisic amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria katika masuala mbalimbali yanayohusu Haki za Binadamu.

Milisic ameipongeza Wizara kwa jitihada za kushirikisha wadau na amesema umoja wa Mataifa utaendelea kutoa ushirikiano ili kufikisha elimu kwa wananchi na kuwezesha zaidi upatikanaji wa haki kwa haraka.

Kikao hicho pia kilihudhuliwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda, Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Bi. Nkasori Sarakikya na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi. Elizabeth Tagora kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA