WAZIRI NDUMBARO ATAKA WANAWAKE WAAMINIWE KUPEWA MADARAKA

 



Waziri Ndumbaro (katikati) akiongea jambo alipokutana na wawakilishi wa WILDAF (kulia).
                                         

Picha ya pamoja.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameitaka jamii ya Tanzania kuwa na Imani na wanawake kuwa wanaweza kushika nafasi za uongozi na kufanya mambo makubwa kwa kuangalia mfano wa anayoyafanya Rais wa sasa wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo wakati alipotembelewa ofisini kwake leo tarehe 30 Mei, 2022 na wawakilishi wa Shirika la wanawake barani Afrika (WILDAF).

Alisema, “Tutumie uwepo wa Rais Samia madarakani kusafisha mawazo ya wasioamini kuhusu wanawake”

Aliongeza, “Tumtangaze na kumpongeza Rais mwanamke kwa kuonyesha anafanya vizuri kwani hii haimjengi Rais Samia bali wanawake wote na viongozi wa sasa na baadae”

Aidha, Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa bado iko kazi kubwa ya kuibadilisha jamii kuhusu mtazamo wao kwa wanawake katika kuweka usawa kuanzia kwenye ngazi ya familia.

Awali akielezea utendaji kazi wa shirika la WILDAF Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo Dkt. Monica Mhoja alisema Shirika lao lina malengo mbalimbali katika kuhakikisha linashiriki katika kumuinua mwanamake ikiwemo kuimarisha upatikanaji haki kwa wanawake na kushawishi utungwaji wa sheria na sera zenye mlengo wa kijinsia na kukuza ufahamu wa haki za wanawake kwa kupunguza ukatili.

Vilevile alibainisha vipaumbele vya Shirika hilo vikiwemo kukuza ufahamu wa wanawake na kupunguza ukatili na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na ngazi za maamuzi.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA