WAZIRI NDUMBARO AZINDUA RASMI KIKOSI KAZI CHA ULINZI KWA WATOTO DHIDI YA BIASHARA YA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amezindua rasmi kikosi kazi cha Ulinzi wa watoto dhidi ya biashara ya Usafirishaji haramu wa binadamu, hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau kutoka katika taasisi na sekta mbali mbali. Dkt. Ndumbaro amesema Wizara ya Katiba na Sheria ndiyo Wizara inayoshughulikia haki za binadamu hivyo siku ya leo ni siku muhimu Sana katika historia ya haki jinai. "Uhalifu huu ni mkubwa sana, ni uhalifu wa kupanga na wa kimataifa, na uko maeneo makubwa, umevuka mipaka, wanasafirisha watoto hususani wasichana." alisema Dkt. Ndumbaro. Aidha, Waziri Ndumbaro amesema mradi huu ni wa miaka minne na kikosi kazi hiki kitajengewa uwezo kuhakikisha kinakabiliana na wahalifu kwa vitendo na kwa kila namna, amesema jukumu la kikosi kazi hiki ni kuwashughulikia wahalifu pamoja na kuha...