Posts

Showing posts from July, 2022

WAZIRI NDUMBARO AZINDUA RASMI KIKOSI KAZI CHA ULINZI KWA WATOTO DHIDI YA BIASHARA YA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amezindua rasmi kikosi kazi cha Ulinzi wa watoto dhidi ya biashara ya Usafirishaji haramu wa binadamu,  hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau kutoka katika taasisi na sekta mbali mbali.     Dkt. Ndumbaro amesema Wizara ya Katiba na Sheria  ndiyo Wizara inayoshughulikia  haki za binadamu  hivyo siku ya leo ni siku muhimu Sana katika historia ya haki jinai.    "Uhalifu huu ni mkubwa sana, ni uhalifu wa kupanga na wa kimataifa, na uko maeneo makubwa, umevuka mipaka, wanasafirisha watoto hususani wasichana." alisema Dkt. Ndumbaro.   Aidha, Waziri Ndumbaro amesema mradi huu ni wa miaka minne na kikosi kazi hiki kitajengewa uwezo kuhakikisha kinakabiliana na wahalifu  kwa vitendo na kwa kila namna, amesema jukumu la kikosi kazi hiki ni kuwashughulikia wahalifu  pamoja na kuhakikisha wahalifu wanaohusika, mkono wa Sheria unachuku

ALIYOSEMA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, DKT. DAMAS NDUMBARO KUHUSU VIPAUMBELE VYA UTEKELEZAJI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KATIKA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2022/2023

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Wizara ya Katiba na Sheria katika mwaka wa fedha 2022/23, Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha bajeti ya jumla ya shilingi 272,768,278,800.00 (Bilioni mia mbili sabini na mbili, milioni mia saba sitini na nane, laki mbili sabini na nane elfu na mia nane) kwa ajili ya Wizara na Taasisi zake ili kuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake.  Katika mwaka wa fedha 2022/2023 bajeti imeongezeka kwa asilimia 18 ya bajeti iliyopitishwa katika Mwaka wa Fedha 2021/22.  Aidha, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara na Taasisi zake itaendelea kuboresha utoaji wa huduma za kisheria kwa Umma ili kuendana na Dhima ya Wizara inayosema kuwa na mfumo madhubuti wa Kikatiba na Sheria wenye kufanikisha utekelezaji wa sera na mipango kwa maendeleo ya Taifa.  Vipaumbele ambavyo Wizara imepanga kutekeleza Mwaka wa Fedha 2022/23 ni pamoja na;*  Kuendelea na kuanza kujenga vituo jumuishi vya Taasisi za Sheria nchini; vituo hivi vitamwezesha mwanachi kupata huduma katik

WAZIRI NDUMBARO ATETA NA KAMISHNA MKUU WA HAKI ZA BINADAMU WA UN

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), amefanya mazungumzo na Bi. Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kubadilishana mawazo juu ya masuala ya haki za binadamu ikiwemo kutolea ufafanuzi tuhuma kuhusu Pori Tengefu la Loliondo na Hifadhi ya  Ngorongoro.  Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 15 Julai 2022, Geneva Uswisi. Kwa upande wake, Bi. Bachelet ameshukuru na kupongeza kwa namna ambavyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza masuala ya haki za binadamu hususan chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika mkutano huo Dkt. Ndumbaro aliambatana na Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva na Mhe. Hoyce Temu, Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Geneva.

SERIKALI MEZANI NA VYOMBO VYA USHAURI VYA UNESCO, WAJADILI KUHUSU MAENEO YA URITHI WA DUNIA

Image
   XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameongoza timu ya wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria kikao cha pamoja na  UNESCO katika Kituo cha Urithi wa Dunia kilichohusisha pia vyombo vya ushauri vya UNESCO yaani IUCN, ICOMOS na ICCROM. Kikao hicho kilifanyika tarehe 13 Julai 2022, Paris Ufaransa.   Katika kikao hicho, ujumbe wa Tanzania umeeleza na kujibu hoja mbalimbali zinazohusu hatua shirikishi za Serikali za kuwaomba na kuwalipa fidia jamii zilizokuwa zinaishi Ngorongoro kisha kuhamia kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni ili kuondoa changamoto za  Uhifadhi wa eneo la Ngorongoro zilizosababishwa na uwepo wa idadi kubwa ya binadamu na mifugo ndani ya eneo la hifadhi, hatua ambayo itaboresha Ikolojia ya eneo hilo na Utalii.    Kwa upande wa Mji Mkongwe wa Zanzibar mazungumzo yalijikita katika Uhifadhi na Maendeleo bila kuathiri Urithi wa Utamaduni.  Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na Mji Mkongwe wa Zanzibar ni miongoni mwa maeneo Saba  ya

KATIBU MKUU MAKONDO AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO WA MANUNUZI KWA MENEJIMENTI YA WIZARA

Image
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akifungua Mafunzo ya Kutumia Mfumo wa Manunuzi (TANePS) kwa Bodi ya Zabuni na Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria, leo tarehe 11 Julai, 2022 Jijini Dar es Salaam.  Mafunzo hayo ambayo yatafanyika hadi tarehe 15 Julai, 2022 ni ya kuwajengea Uwezo Wakuu wa Idara na Vitengo katika masuala ya matumizi ya Mfumo wa Manunuzi. Katibu Mkuu Makondo alitoa maelekezo kwa Washiriki kuhakikisha wanayatumia Mafunzo hayo kujifunza na kushiriki kikamilifu kwa kutumia uzoefu wao katika kazi na matumizi ya mfumo katika kusaidia shughuli za Serikali.

UZINDUZI WA KIKOSI KAZI CHA KUPAMBANA NA UHALIFU MKUBWA WA KUPANGWA

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo akizungumza katika  hafla ya uzinduzi Kikosi Kazi  kilichoundwa na Serikali kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa, hususani usafirishaji haramu wa binadamu na udhalilishaji wa kingono kwa watoto. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar. Uzinduzi ulifanyika Zanzibar tarehe 6 Julai, 2022

KATIBU MKUU MAKONDO, UNICEF WAJADILI NAMNA YA KUIMARISHA ULINZI WA HAKI ZA MTOTO

Image
   XXXXXXXXXXXXXX Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amekutana na ujumbe wa wawakilishi kutoka UNICEF ukiongozwa na Mkuu wa Ulinzi wa Mtoto, Bi. Maud Droogleever Fortuijn na kujadili namna watakavyoshirikiana  kuimarisha ulinzi wa haki kwa mtoto.   Bi. Makondo amewahakikishia UNICEF kuwa Wizara ya Katiba na Sheria itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa,  Aidha ameahidi kuwa wadau watashirikishwa katika hatua zote za maboresho ya mfumo wa haki jinai.   Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za RITA Jijini Dar es Salaam, tarehe 8 Julai, 2022.  

SERIKALI YAZUNGUMZA NA WATAALAM WA HAKI ZA BINADAMU (SPECIAL RAPPORTEURS) WA UMOJA WA MATAIFA

Image
   XXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro ameongoza kikao na Wataalam wa Haki za Binadamu (Special Rapporteurs) wa Umoja wa Mataifa wanaoshughulikia masuala ya watu asilia (indigenous people) na makazi.   Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kawaalika nchini Tanzania wataalam hao wa haki za binadamu   "kwa niaba ya Serikali nawakaribisha sana mje kutembelea Tanzania na mpate fursa ya kujionea vivutio vya utalii, tamaduni zetu na utofauti wa mila mbalimbali za makabila zaidi ya 100 yaliyopo Tanzania" alisema Dkt. Ndumbaro   Wataalam hao wamepongeza jitihada za Serikali katika kutekeleza haki za binadamu hususani fidia waliyowapatia waliokuwa wakazi wa Ngorongoro na kuhamia Msomera wilayani Handeni kwa hiyari yao. Aidha, wameahidi ushirikiano zaidi na Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu.   Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 8 Julai, 2022 jijini Arusha, ulihudhuriwa pia na Katibu Mk

WANANCHI MSISUBIRI MATUKIO YA KITAIFA PEKEE KUTAFUTA HUDUMA KWANI VYETI VYA KUZALIWA VINATOLEWA SIKU ZOTE- WAZIRI NDUMBARO

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXX   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro leo tarehe 6 Julai ,2022 ametembelea na kukagua zoezi la usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa Wananchi linaloendelea katika viwanja vya Maonesho ya biashara ya Kimataifa Sabasaba Jijini Dar es salaam.   Akiongea na Wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma hiyo Mhe, Dkt Ndumbaro amewataka kuwa mabalozi watakaporudi majumbani mwao Kwa kuwaeleza ndugu, jamaa na majirani zao kuhusu umuhimu wa kusajili amatukio ya vizazi na vifo, ndoa na talaka na mengineyo kwa wakati badala ya kusubiri maonesho au matukio yanayowakusanya kwa mwaka mara moja.   ‘’Sasa hivi huduma zimesogezwa karibu yenu kwa upande wa watoto wa umri chini ya miaka mitano wanasajiliwa katika ofisi za kata na vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya mama na mtoto katika Mikoa 23 na kwa upande wenu watu wazima unaweza kujisajili kielektroniki sehemu yoyote ulipo Kisha ukapata cheti chako Kwa wakati muafaka’’ Alisema Mhe. Dkt Ndumbaro.   Kwa upande

WAZIRI NDUMBARO AFUNGUA MAFUNZO YA SHERIA YA MANUNUZI KWA BODI YA ZABUNI NA MENEJIMENTI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefungua mafunzo ya Sheria ya Manunuzi kwa Bodi ya Uzabuni na Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria. Mafunzo haya yameaza leo tarehe 6-9 Julai, 2022 Jijini Dar es salaam. Dkt. Ndumbaro amesema mafunzo haya yaangalie na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ili kuboresha mfumo wa manunuzi na kuondoa urasimu "kama wataalam tutafute fomula itakayotupa mfumo wenye uwazi, thamani ya pesa, ubora wa bidhaa na huduma na kuondoa mianya ya rushwa pasipo kuwepo kwa urasimu" alisema Dkt. Ndumbaro

KIKAO CHA DHARURA CHA 6 CHA KAMATI YA MAWAZIRI WA MASUALA YA HAKI NA SHERIA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Wataalam kutoka Wizara ya Katiba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Wizara ya Afya katika kikao cha dharura cha 6 cha kamati ya Mawaziri wa Masuala ya Haki na Sheria cha Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya kupitisha marekebisho ya sheria ya kuundwa Taasisi ya Afrika kudhibiti na kuzuia magonjwa (Afrika CDC) kilichofanyika kwa njia ya mseto kutoka Adis Ababa Ethiopia, Julai 4, 2022

KISWAHILI KINAFANYA MAHAKAMA KUTEMBEA ‘KIFUA MBELE’

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akipokea  maandamano ambayo yanahusu Kiswahili na haki kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Utamaduni Duniani (MASIKIDU).    Maandamano yakipita mbele ya Waziri Ndumbaro.  XXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema mwelekeo wa Serikali katika kukiendeleza Kiswahili unafanya Mahakama kutembea ‘kifua mbele’ kwa kuzingatia usemi wa “Thamini chako”.    Mhe. Ndumbaro amesema hayo Julai 4, 2022 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam wakati anapokea maandamano ambayo yanahusu Kiswahili na haki kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Utamaduni Duniani (MASIKIDU).    “Kiswahili chetu tu, ndicho tunachopaswa kujivunia kila siku, lugha za wengine siyo zetu. Kwa hiyo, Kiswahili ndiyo lugha pekee ambayo imetufanya Watanzania kwa miaka sitini ya uhuru, kuishi pamoja na kufanya shughuli zetu kwa undugu, utulivu, amani na umoja.   Hatua hiyo imekifanya Kiswahili kupigiwa upatu kitumike katika masuala yote ya kisheria

MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YAWE ENDELEVU - WAZIRI NDUMBARO

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) , Waziri wa Katiba na Sheria amesema mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanatakiwa kuwa endelevu. Dkt. Ndumbaro amesema hayo kwa niaba ya Mhe. George Simbachachene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) wakati akimkaribisha Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufunga rasmi maadhimsho ya kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika tarehe 1-2 Julai, 2022 Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. "Dawa za kulevya zina madhara makubwa kwa ustawi wa jamii, Maendeleo ya Nchi na Dunia kwa ujumla, hivyo mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya yanatakiwa kuwa endelevu" alisema Dkt. Ndumbaro.

Kikao cha Uwasilishaji wa Andiko la Utekelezaji wa Mradi wa Kupambana na Uhalifu Mkubwa wa Kupangwa.

Image
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria akiongoza kikao cha uwasilishaji wa andiko la Utekelezaji wa Mradi wa Kupambana na Uhalifu Mkubwa wa Kupangwa. Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatib Kazungu akifafanua jambo kwenye kikao hicho Washiriki wa kikao. XXXXXXXXXXXXXX Kikao cha uwasilishwaji wa Andiko la Utekelezaji wa Mradi wa Kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa. Kikao kimefanyika Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria mtumba jijini Dodoma Julai 1, 2022 na kiliongozwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo na kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu  TAMISEMI Dkt. Charles Msonde na Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Bw. Christopher Kadio, Pia Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu.

WAZIRI NDUMBARO ATAKA KASI YA UJENZI JENGO LA WIZARA IONGEZWE

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro, akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Juni 30, 2022. Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro, akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa  Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo  katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Juni 30, 2022. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Geophrey Pinda, akizungumza mara baada ya Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Juni 30, 2022. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo, akimshukuru Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro kwa kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Juni 30, 2022. XXXXXX